Sunday, December 2, 2012
KOCHA wa Rwanda, Mserbia Milutin Sredojevic ‘Micho’ ameonyesha dalili za kutosha kwamba anaiogopa Tanzania Bara kuelekea mchezo wa Robo Fainali, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge kesho Uwanja wa Lugogo mjini hapa.Akizungumza baada ya mechi ya jana, Micho alisema kwamba kuelekea mchezo wa kesho Tanzania wana nafasi nzuri kwa sababu jana walikuwa mazoezini dhidi ya Somalia, wakati Rwanda walikuwa wana mechi ngumu na Eritrea.“Walikuwa mazoezini tu na Somalia, wamepumzika zaidi, sisi tumecheza mechi ngumu, tena napenda niseme dhidi ya timu ambayo imecheza soka ya kuvutia zaidi katika mashindano haya. Nawapongeza (Eritrea) kwa hilo,”alisema Micho.Pamoja na hayo, Micho aliisifu timu yake kwamba daima katika mashindano haya huwa haitolewi katika hatua ya makundi na jana imeendeleza utamaduni huo, baada ya kufuzu Robo Fainali.Micho alisema anaiheshimu Tanzania ni timu nzuri na anatarajia mchezo utakuwa mgumu, lakini watapigana kwa nguvu zao zote kuhakikisha wanashinda na kwenda Nusu Fainali.Bara, Kilimanjaro Stars itacheza na Rwanda katika Robo Fainali ya CECAFA Tusker Challenge kesho kwenye Uwanja wa Lugogo kuanzia saa 8:00 mchana, wakati Zanzibar itacheza na Burundi saa 10:00 jioni.Robo Fainali nyingine zitachezwa Jumanne Uwanja wa Mandela, Namboole, kati ya Kenya na Malawi saa 10:00 jioni wakati wenyeji Uganda watacheza na Ethiopia saa 1:00 usiku.Katika mechi za jana, Bara iliilaza Burundi mabao 7-0 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Lugogo mjini hapa. Matokeo hayo yanaifanya Bara itimize pointi sita baada ya kucheza mechi tatu na sasa, wakishinda mbili na kufungwa moja.Burundi imemalizaa kileleni mwa Kundi B, kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Sudan, bao pekee la Chris Nduwarugira jana. Rwanda iliifunga Eritrea 2-0, mabao ya Tadi Etikiama na Tumaine Ntamuhanga, huku Malawi ikiilaza Zanzibar 2-0.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment