KIPA wa zamani wa Simba na aliyekuwa kocha wa makipa wa timu hiyo, Iddi Pazi ‘Father’ amesema kwamba uwezo wa kipa namba moja wa sasa klabu hiyo umeshuka na tiba yake anaijua.“Kaseja uwezo umeshuka kidogo, kwa sababu daktari wake sipo pale, Simba wakinirudisha kazini, Kaseja atafufua makali yake na atakuwa hafungiki kwa urahisi,”alisema Pazi.Pazi ameushauri uongozi wa Simba umerejeshe kazini ili aokoe kipaji cha kipa huyo bora, miongoni mwa walinda milango bora kuwahi kutokea Tanzania.Kwa sasa, kocha wa makipa wa Simba ni kipa mwingine wa zamani wa Simba, James Kisaka ambaye alipewa kazi hiyo baada ya Pazi kwenda Oman. Lakini kwa sasa Pazi amemaliza mkataba wake Oman na yupo nyumbani kwake, Majumba Sita, Ukonga, Dar es Salaam.Katika mechi 12, Kaseja amefungwa mabao 10 kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzanoia Bara msimu huu, kitu ambacho si kawaida yake katika misimu iliyotangulia, ingawa hiyo inaelezwa inachangiwa hata na ubutu wa safu ya ulinzi ya sasa wa timu hiyo.Lakini pia, kocha Mserbia wa Simba SC, Profesa Milovan Cirkovick naye anadaiwa kuchangia matokeo mabaya na habari zinasema anaweza kutimuliwa wakati wowote kwenye klabu hiyo, kufuatia kutofautiana na uongozi wa klabu hiyo.Uongozi wa Simba unamtuhumu Mserbia huyo kwamba ni mbishi hashauriki na hilo limekuwa likiigharimu timu katika michezo yake ya karibuni ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.“Huyu jamaa tumemvumilia sana, mimi sina hamu naye tena, sijui wenzangu. Anapanga kikosi ovyo na ndiyo chanzo cha matokeo haya mabaya,”alisema kiongozi mmoja wa Simba. Lakini kwa upande mwingine, inadaiwa matokeo haya mabaya ya Simba ni matokeo ya mgomo wa wachezaji wakishinikiza wachezaji wenzao waliosimamishwa Haruna Moshi ‘Boban’ na Juma Nyosso warejeshwe kikosini.Zaidi Boban, wachezaji wanadaiwa kumpenda sana kutokana na roho yake safi ya kibinadamu na upendo mkubwa kwa wenzake.Boban ndiye mchezaji pekee aliyejitolea kuusindikiza nyumbani kwao, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) mwili wa marehemu Patrick Muteesa Mafisango, kiungo wa Simba aliyefariki dunia Mei mwaka huu kwa ajali ya gari.Simba SC juzi ilifungwa mechi ya kwanza ya Ligi Kuu mabao 2-0 na Mtibwa Sugar, Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, mabao ya Said Mkopo na Hussein Javu.Simba inabaki na pointi zake 23, baada ya kucheza mechi 12, ikiipisha kileleni Yanga yenye pointi 26 sasa. Simba itamaliza mzunguko wa kwanza wa ligi kwa kumenyana
No comments:
Post a Comment