KENYA
wako hatarini kupokonywa uenyeji wa Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na
Kati, CECAFA Tusker Challenge mwakani na badala yake wakapewa Rwanda.
Habari
kutoka kwenye Mkutano wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati
(CECAFA) uliofanyika Ijumaa iliyopita, zimesema kwamba Rwanda wameambiwa wakae
tayari kwa uenyeji wa michuano hiyo, iwapo Kenya itachemsha.
Habari
zinasema Mwenyekiti wa Shirikiasho la Soka Kenya (FKF), Sam Nyamweya, awali
alisema katika Mkutano Mkuu wa CECAFA kwenye hoteli ya Serena, kwamba Kenya
tayari imekwishapata mfadhili wa mashindano hayo.
Kasha
baadaye, Mwenyekiti wa Shirikisho la Soka Rwanda, FERWAFA, Celestin Ntagungira,
akasema itakuwa tayari kutaja jina la mdhmaini wa Challenge ndani ya wiki mbili
wakipewa uenyeji.
Katika
kuamua utata huo, Rais wa CECAFA Injinia Leodegar Tenga alisema haki za uenyeji
wa Challenge ya mwakani zitakwenda kwa nchi ambayo kwanza itawahakikishia
mdhamini wa mashindano.
No comments:
Post a Comment