habari

MATANGAO

Tuesday, November 27, 2012


KENYA wako hatarini kupokonywa uenyeji wa Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge mwakani na badala yake wakapewa Rwanda.
Habari kutoka kwenye Mkutano wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) uliofanyika Ijumaa iliyopita, zimesema kwamba Rwanda wameambiwa wakae tayari kwa uenyeji wa michuano hiyo, iwapo Kenya itachemsha.
Habari zinasema Mwenyekiti wa Shirikiasho la Soka Kenya (FKF), Sam Nyamweya, awali alisema katika Mkutano Mkuu wa CECAFA kwenye hoteli ya Serena, kwamba Kenya tayari imekwishapata mfadhili wa mashindano hayo.
Kasha baadaye, Mwenyekiti wa Shirikisho la Soka Rwanda, FERWAFA, Celestin Ntagungira, akasema itakuwa tayari kutaja jina la mdhmaini wa Challenge ndani ya wiki mbili wakipewa uenyeji.
Katika kuamua utata huo, Rais wa CECAFA Injinia Leodegar Tenga alisema haki za uenyeji wa Challenge ya mwakani zitakwenda kwa nchi ambayo kwanza itawahakikishia mdhamini wa mashindano.

RAIS wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Leodger Tenga amewataka wachezaji wa timu hiyo kuachana na fikra ya kuwa wapinzania wao, Congo Brazaville inaundwa na wachezaji waliozidi umri ‘Vijeba’ , badala yake vijana hao wajitume ili ushindi upatikane.Hatua hiyo inafuatia kuwepo kwa malalamiko ya Congo Brazavile kuchezesha Vijeba katika mechi yao ya awali ya kuwania kucheza fainali za Afrika wiki iliyopita jijini Dar es Salaam ambapo Serengeti ilishinda bao 1-0.Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Tenga alisema haoni sababu ya kuwakatia rufaa kama ilivyoelezwa awali, kwani tayari walisharipoti kwa kamishna wa mchezo huo na kama watafanya hivyo itakuwa baadaye.Alisema wachezaji hao hawana budi kuelekeza akili zao kwenye mechi ya marudiano itakayopigwa ugenini mwishoni mwa wiki hii na kuhakikisha wanashinda ili kusonga mbele. “Nisingependa hili neno la Vijeba liingie katika akili za hawa watoto ili waende kupambana na kurudi na ushind,”alisema.Aidha, Tenga amewapongeza vijana hao kwa ushindi walioupata katika mchezo wao wa awali licha ya kuwa ni finyu na kuwataka kuendelea na moyo wa kujituma ili waweze kufika mbali. “Pia TFF inashukuru mashabiki waliojitokeza kwa wingi kuja kuishangilia timu yao, sambamba na kamati ya kuisaidia Serengeti kwa mchango wao wa hali na mali,”alisema.Katika hatua nyingine, Tenga ametolea ufafanuzi suala la mgawo wa sh mil 1 kati ya mil 23 zilizopatikana katika mchezo wa Serengeti Boys na wenzao wa Congo Brazaville baada ya kamati ya kuisaidia Serengeti ambayo ilichanga milioni 35 kulalamika.Tenga alisema mil.35 zilizochangwa na kamati hiyo zilitumika kufidia hasara iliyopatikana katika mchezo huo kwani mchezo unaofanyika katika uwanja wa Taifa na kuingiza chini ya mil.80 ni lazima TFF ibaki na madeni. “Ndiyo maana tumekuwa tuklipeleka mechi bndogondogo na zile za vijana katika uwanja wa Uhuru kwa sababu ya gharama za Uwanja wa Taifa, lakini kutokana na uwanja wa Uhuru kutotumika ndo hatuna dudi kubaki Taifa na matokeo yake ndiyo kama hivyo.”alisema Tenga.Tenga aliongeza kwamba, mara nyingi TFF imekuwa ikipata mzigo wa kulipa madeni yanayotokana na hasara za michezo mbalimbali inayofanyika kwenye uwanja wa Taifa.Tenga alisema kwa sasa timu hiyo inatakiwa kuendelea kujengwa kisaikolojia ili iweze kuwa katika hali nzuri na kufanikisha malengo yake ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya soka la Tanzania.Kikosi cha wachezaji 18 na viongozi saba wa Serengeti Boys kinatarajiwa kuondoka nchini kesho kwenda Congo Brazzavile tayari kwa mchezo huo.

Monday, November 26, 2012


KATIKA kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga ya Dar es Salaam inatarajia kwenda kuweka kambi ya wiki mbili nchini Uturuki mapema mwakani.Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Abdallah Ahmad Bin Kleb amesema leo katika Mkutano na Waandishi wa Habari, makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam kwamba ziara hiyo inatarajiwa kufanyika kati ya Desemba na Februari 25, mwakani.Alisema pendekezo la kambi hiyo lilitolewa na kocha mkuu wa Yanga, Mholanzi Ernie Brandts ambaye ana uzoefu na nchi hiyo ambayo ina vitu vinavyostahili kwa ajili ya timu kuweka kambi.Alisema ikiwa huko timu hiyo inatarajiwa kucheza mechi mbili za kitrafiki na timu zitkazotajwa baadaye.Aidha, kocha mkuu wa timu hiyo amewapandisha wachezaji watatu wa kikosi cha vijana chini ya  miaka 20 wakiwemo kipa, Yussuf Abdallah, George Banda na Rehan Kibinga.Katika hatua nyingine, Bin Kleb aliasema wanajivunia uongozi wa sasa chini ya Mwenyekiti, Alhaj Yussuf Manji, kwani timu imekuwa na mafanikio makubwa ikiwemo kutwaa kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kagame, kufanya vema katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ambao ulimalizika kwa timu  kuongoza.Alisema kufanya vizuri katika Ligi Kuu, ni matunda ya timu hiyo kuweka kambi nchini Rwanda baada ya Kombe la Kagame


ZANZIBAR HEROES YAANZA DROO KATIKA MASHINNDANO  YA CHALLENGE CUP.
ZANZIBAR HEROES YAANZA DROO KATIKA MASHINNDANO  YA CHALLENGE CUP.

NA USHINDI WA MABAO2-0,MAGOLI ALIYEFUNGA NI MSHAMBULIAJI WA, WA TIMU YA YOUNG AFRICAN SPORT CLUB NIYONZIMA DAKIKA 79.
TIMU YA RWNANDA ILIYOKO KATIKA  MASHINDANO LEO  IMEWEZA KUIBUKA NA USHINDI WA MABAO2-0,MAGOLI ALIYEFUNGA NI MSHAMBULIAJI WA, WA TIMU YA YOUNG AFRICAN SPORT CLUB NIYONZIMA DAKIKA79

Sunday, November 25, 2012


PICHA ZA TAIFA STARS  NA SUDAN KATIKA UWANJA WA KAMPALA UGANDA, LEO TIMU YA TAIFA STARS IMEIBUKA NA USHINDI WA MABAO2-0,YAKIWEKWA NA JOHN BOCCO, MRISHO NGASA AKIWA ANATOA KROSI NA PASI.


JOHN BOCCO,NDIYE ALIYEFUNGA MAGOLI YOTE2-0.
MSUVA AKIMTOKA MCHEZAJI WA SUDAN. 


MASHABIKI WA TANZANIA WAKIJA KUWAPA SUPPORT TIMU YAO.
TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania Bara, imeanza vema kampeni zake za kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge, baada ya kuichapa mabao 2-0 Sudan katika mchezo uliomalizika usiku huu kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole, Kampala, Uganda.
Ushindi huo, unaiweza Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Kundi B, nyuma ya Burundi inayoongoza kwa wastani wa mabao.
Hadi mapumziko, Stars walikuwa mbele kwa mabao 2-0, yote yakipachikwa kimiani na mshambuliaji wa Azam FC, John Raphael Bocco ‘Adebayor’ aliyetumia vema krosi za Mrisho Khalfan Ngassa.
Bocco alifunga bao la kwanza Bocco aliiwahi vema krosi ya Ngassa aliyewatoka mabeki wa Sudan wingi ya kushoto na kuitumbukiza kimiani dakika ya 14.
Adebayor wa Chamazi aliwainua tena vitini mashabiki wa Tanzania dakika ya 28, akiunganisha krosi ya Ngassa tena kutoka kule kule kushoto.
Kwa ujumla Tanzania Bara walicheza vizuri kipindi cha kwanza, wakishambulia zaidi kupitia pembeni, kulia Simon Msuva ambaye hakuwa na madhara sana na kushoto Ngassa ambaye alikuwa mwiba mchungu haswa kwa Wasudan.
Pamoja na Bara kutawala kipindi cha kwanza, lakini Wasudan walifanya mashambulizi kadhaa ya kushitukiza na sifa zimuendee mlinda mlango Juma Kaseja, ambaye alioko amichomo miwili ya hatari mno.
Kipindi cha pili Stars, inayofundishwa na Mdenmark Kim Poulsen iliendelea kutawala mchezo, lakini safu ya ulinzi ya Sudan iligangamala.
Tanzania Bara; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Amir Maftah, Shomari Kapombe, Kevin Yondan, Frank Domayo, Salum Abubakar/Amri Kiemba, John Bocco, Mwinyi Kazimoto na Simon Msuva/Shaaban Nditi.
Sudan; Ebd Elrahman Ali, Moawia El Amin, Sami Abdallah, Faris Abdallah, Hamoda Bashir/Farid Mohamed, Mohamed El Mortada, Sadam Abutalib, Mohamed Mussa Idris, Modathir Mohamed, Adam Sayer/Osama El Rashid na Mohamed Osman/Saed Siddig.
Katika mchezo wa awali, Burundi walishinda mabao 5-1, mabao yake yakifungwa na Chris Nduwarugira dakika ya 35 na 88, Yussuf Ndikumana dakika ya 41 na Suleiman Ndikumana dakika ya 84 na 90, wakati la Somalia lilifungwa na Mohamed Jabril kwa penalti dakika ya 55.
Matokeo hayo yanalifanya Kundi B lizidi kuwa gumu, kwani Burundi inaongoza kwa pointi zake tatu na mabao mengi, Tanzania ya pili kwa pointi tatu na mabao mawili- lakini bado Sudan wanaweza kupata matokeo mazuri katika mechi zijazo.
                    NENO LA LEO LANGU

MUNGU BARIKI TANZANIA MUNGU BARIKI WACHEZAJI WAKE.

Saturday, November 24, 2012


TIMU ya taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars imelalamikia Uwanja mbovu wa Chuo Kikuu cha Kampala Kampasi ya Biashara, waliopelekwa kufanya mazoezi leo kujiandaa na mechi ya kesho ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge 2012 dhidi ya Sudan, itakayopigwa kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole mjini hapa.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace Wambura amewasilisha malalamiko hayo kwa Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Uganda (FUFA), Rodgers Mulindwa ambaye ameahidi kuyafanyia kazi.
“Tutalifanyia kazi suala hilo, tutakuwa na kikao kesho litawasilishwa na litapatiwa usumbufu, mwanzo huwa na matatizo, lakini mambo yatakuwa mazuri,”alisema Mulindwa.
Hata hivyo, inashangaza Stars kupelekwa katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Kampala Kampasi ya Biashara, wakati kwenye mpango wa awali kabisa wa FUFA ilitakiwa kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Nakawa.
Kwa upande wake, kocha wa Kilimanjaro Stars, Mdenmark Kim Poulsen amesikitishwa na kutowasili kwa washambuliaji Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
“Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaweza wasicheze katika mechi ya kesho kwa sababu hawajafika, lakini mimi nikiwa kocha nimejiandaa vizuri na nina imani na wachezaji waliopo,” alisema.
“Nina imani TFF wanafuatilia suala hili na wachezaji hawa watajiunga na wenzao hivi karibuni lakini hii haituzuii kufanya vizuri kwani tumejiandaa vizuri,” alisema.
Alisema wachezaji wote wana hali nzuri na wana ari ya kushinda mechi yao ya kwanza dhidi ya Sudan ambazi zimo katika Kundi B pamoja na Burundi na Somalia 

Friday, November 23, 2012


MAMBO yameiva Yanga- matumaini ya wapenzi wa klabu hiyo kushuhudia klabu yao ikiwa na Uwanja mpya wa kisasa yameanza kuonyesha dalili za kutimia, kufuatia uongozi wa klabu hiyo kusaini makubaliano ya awali na Kampuni ya Beijing Construction Engineering Group iliyojenga Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja wa Kaunda.Mwenyekiti wa mabingwa hao wa Afrika Mashariki na Kati, Alhaj Yussuf Mehboob Manji leo amesaini makubaliano na Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo, David Zhang, makao makuu ya klabu hiyo, makutano ya mitaa ya Jangwani na Twiga, Dar es Salaam.Katika makubaliano hayo, ujenzi huo wa Uwanja utakaokuwa na uwezo wa kuchukua mashabiki 30,000 hadi 40,000 utaanza rasmi Juni mwakani.Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa kusaini makubaliano hayo leo mchana, Alhaj Manji alisema kwamba wanfurahi kuanza safari ya ujenzi wa Uwanja wao na anaamini huo ni mwanzo wa mzuri wa mipango yao ya kuifanya Yanga ijitegemee kiuchumi.Katika hatua nyingine, Manji amesema kwamba katika mipango yao ya kuifanya Yanga ijimudu kiuchumi, wanafikiria kulikarabati pia jengo dogo la klabu hiyo, liliopo Mtaa wa Mafia.Alhaj Manji alisema Jumatatu kampuni hiyo ya ujenzi kutoka China, ambayo ndiyo iliyojenga Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam itachukua vipimo kwenye Uwanja wa Kaunda na Uongozi wa Yanga kuliwasilisha suala la ujenzi huo kwenye Mkutano Mkuu wa Wanachama wa klabu hiyo, Desemba 8, mwaka huu.Alisema baadhi ya fedha kwa ajili ya uwanja huo wa kisasa watakapo benki na gharama nyingine zitatokana na michango ya wanachama baada ya kuwa wamepata gharama nzima za ujenzi za uwanja huo.Meneja Mkuu wa Kampuni ya Beijing Cobnstruction Engineering Group alisema wanafurahia kufikia makubaliano ya awali ya ujenzi wa uwanja na klabu ya Yanga.Alisema wao ndio walijenga Uwanja wa Taifa na viwango vya ujenzi vya uwanja huo vilisifiwa na timu ya taifa ya Brazil iliyokuja kucheza mechi ya kirafiki na Tanzania mwaka 2010 ikiwa njiani kuelekea Afrika Kusini ambako fainali za kombe la Dunia zilifanyika.

Sunday, November 11, 2012


PICHA ZA SIMBA SPORT CLUB NA TOTO AFRICAN JANA WALIVYOBANWA SIMBA KATIKA UWANJA WA DAR-ES -SALAAM,TOTO AFRICAN WAKI UBUKA NA USHINDI WA 1-0.