habari

MATANGAO

Monday, December 10, 2012



KOCHA wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametangaza kikosi cha wachezaji 24 kitakachoingia kambini jioni ya Desemba 12 mwaka huu kuajianda kwa mechi ya kirafiki dhidi ya mabingwa wa Afrika, Zambia.

Katika kikosi hicho, wachezaji walioitwa kwa mara ya kwanza ni kipa Aishi Manula anachezea kikosi cha U20 cha Azam na timu ya Taifa kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes), beki wa kushoto wa Azam, Samih Nuhu, beki wa kushoto wa Mtibwa Sugar, Issa Rashid na mshambuliaji wa Azam, Mcha Khamis.

Pia kati ya wachezaji walioitwa, sita walikuwa kwenye kikosi cha Zanzibar (Zanzibar Heroes) kilichokamata nafasi ya tatu katika michuano ya Kombe la Chalenji iliyomalizika Jumamosi jijini Kamapala, Uganda. Wachezaji hao ni Mwadini Ally, Nassoro Masoud Cholo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Samih Nuhu, Aggrey Morris na Mcha Khamis.

Kikosi kamili kilichoitwa ni makipa; Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ally na Aishi Manula (Azam U20). Mabeki ni Shomari Kapombe (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Nassoro Masoud Cholo (Simba), Aggrey Morris (Azam), Samih Nuhu (Azam), Nadir Haroub ‘Cannavaro’ (Yanga), Amir Maftah (Simba), Issa Rashid (Mtibwa Sugar) na Kevin Yondani (Simba).

Viungo ni Frank Domayo (Yanga), Athuman Idd Chuji (Yanga), Mrisho Ngasa (Simba), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Mcha Khamis (Azam), Salum Abubakar (Azam), Amri Kiemba (Simba) na Mbwana Samata (TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo- DRC).

Washambuliaji ni John Bocco (Azam), Simon Msuva (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC) na Mwinyi Kazimoto (Simba).

Monday, December 3, 2012

KIKOSI CHA TANZANIA-TAIFA STARS.



KIKOSI CHA RWANDA.
KIPA JUMA KASEJA AKISALIMIANA NA NIYONZIMA.
KIPA JUMA KASEJA AKIUDAKA MPIRA  KATIKA LANGONI MWAKE.
MASHABIKI WA TAIFA STARS WAKIMPONGEZA KUFUNGA BAO LA PILI.
WATU WALIO KUJA KUISHANGILIA TAIFA STARS. 
MCHEZAJI WA TAIFA ALIFANYIWA MADHAMBI.
ATHUMANI IDDAKIUPIJA MPIRA KWA KICHWA ULIO CHINI.
AMIR KIEMBA ANAMTOKA MCHEZAJI WA RWANDA KWA CHENGA.
KOCHA WA RWANDA AKICHANGAYIKIWA KWA MAGOLI YALIO FUNGWA NA  TAIFA STARS.
JOHN BOCCO AKIGOMBANIA MPIRA NA WA CHEZAJI WA RWANDA.
AMIR KIEMBA AKISHANGILIA  WAKATI NGASA AKIWA NYUMA YAKE.
GOLI ALIYE FUNGA AMIR KIEMBA BAO LA KWANZA-1-0.
MWINYI KAZI MOTO AKIMTOKA MCHEZAJI WA RWANDA.
JOHN BOCCCO AKIACHIA SHUTI  HAPA.
GOLI KIPA WA RWANDA AKIRUKA JUUU  KUOKOA  HATARI LANGONI  MWAKE.
MWINYI KAZI MOTO AKIWATOKA DAKIKA ZIKIWA ZAMWISHO HAPA90.

KIKOSI CHA TAIFA STARS.
KIKOSI CHA RWANDA.
KIPA JUMA KASEJA AKISALIMIANA  NA NIYO NZIMA.
TANZANIA Bara imefanikiwa kuingia Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ya afrika Mashariki na kati, CECAFA Tusker Challenge baada ya kuilaza Rwanda mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Lugogo mjini hapa mchana huu.
Hadi mapumziko, Stars walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililotiwa kimiani na kiungo Amri Kiemba, dakika mya 33 akiunganisha pasi ya Mwinyi Kazimoto aliyewapunguza wachezaji wawili wa Rwanda kabla ya kutoa pasi maridadi.
Katika mechi hiyo iliyochezeshwa na refa Mohamed El Fadil kutoka Sudan, mshambuliaji John Raphael Bocco ‘Adebayor’ alikuwa mwiba mchungu kwa safu ya ulinzi ya Rwanda na aliwafanya waende kwenye vyumba vya kupumzikia wakiwa hoi.
Katika hicho kipindi cha kwanza, Rwanda walikosa bao la wazi dakika ya 12 baada ya krosi ya Jean Claude Iranzi kuokolewa na beki Kevin Yondan kwa kichwa na dakika ya 19 Jean Baptiste Mugiraneza alipiga juu akiwa nje kidogo ya eneo la hatari.
Stars pamoja na kufunga bao hilo kipindi hicho cha kwanza, katika dakika ya 30 krosi nzuri ya  Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Mrisho Ngassa na Bocco walishindwa kuiunganisha na ikawapita wote.
Ngassa tena, katika dakika ya 38 alipiga shuti kali kutoka wingi ya kushoto, lakini likaenda  nje sentimita chache.
Kipindi cha pili,
Kipindi cha pili Stars walirudi vizuri tena na kuendelea kucheza kwa kuonana, ingawa na Rwanda nao waliendelea kucheza kwa bidii kutafuta bao la kusawazisha.
Hata hivyo, walikuwa ni Stars tena waliofanikiwa kupata bao la pili 53 baada ya John Bocco kuuwahi mpira uliotemwa na kipa Jean Claude Ndoli kufuatia shuti kali la Mwinyi Kazimoto kutoka nje ya eneo la hatari.
Baada ya bao hilo, Rwanda walionekana kupagawa, lakini hawakusahau kushambulia lango la Stars na dakika ya 86 Dadi Birori hakujali ameotea akasukuma mpira nyavuni, lakini refa akakataa bao hilo.
Kwa ushindi huo, Stars sasa inasubiri mshindi kati ya Uganda na Ethiopia kesho kukutana naye  kwenye Nusu Fainali.
Stars; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Amir Maftah, Shomary Kapombe, Kevin Yondan, Amri Kiemba, Salum Abubakar/Athumani Iddi dk51, Frank Domayo, Mwinyi Kazimoto, Mrisho Ngassa na John Bocco/Shaaban Nditi dk 85.
Rwanda; Jean Claude Ndoli, Emery Basiyenge, Ismail Nshutimayamangara/Fabrice Twagizimana dk19, Jimmy Mbaraga/Imran Nshiyimana dk67, Charles Tibingana/Barnabe Mbuyumbyi dk61, Michel Rusheshangoga, Jean Baptiste Mugiraneza, Haruna Niyonzima, Jean Claude Iranzi, Dadi Birori na Tumaine Ntamuhanga.

Sunday, December 2, 2012


KOCHA wa Rwanda, Mserbia Milutin Sredojevic ‘Micho’ ameonyesha dalili za kutosha kwamba anaiogopa Tanzania Bara kuelekea mchezo wa Robo Fainali, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge kesho Uwanja wa Lugogo mjini hapa.Akizungumza baada ya mechi ya jana, Micho alisema kwamba kuelekea mchezo wa kesho Tanzania wana nafasi nzuri kwa sababu jana walikuwa mazoezini dhidi ya Somalia, wakati Rwanda walikuwa wana mechi ngumu na Eritrea.“Walikuwa mazoezini tu na Somalia, wamepumzika zaidi, sisi tumecheza mechi ngumu, tena napenda niseme dhidi ya timu ambayo imecheza soka ya kuvutia zaidi katika mashindano haya. Nawapongeza (Eritrea) kwa hilo,”alisema Micho.Pamoja na hayo, Micho aliisifu timu yake kwamba daima katika mashindano haya huwa haitolewi katika hatua ya makundi na jana imeendeleza utamaduni huo, baada ya kufuzu Robo Fainali.Micho alisema anaiheshimu Tanzania ni timu nzuri na anatarajia mchezo utakuwa mgumu, lakini watapigana kwa nguvu zao zote kuhakikisha wanashinda na kwenda Nusu Fainali.Bara, Kilimanjaro Stars itacheza na Rwanda katika Robo Fainali ya CECAFA Tusker Challenge kesho kwenye Uwanja wa Lugogo kuanzia saa 8:00 mchana, wakati Zanzibar itacheza na Burundi saa 10:00 jioni.Robo Fainali nyingine zitachezwa Jumanne Uwanja wa Mandela, Namboole, kati ya Kenya na Malawi saa 10:00 jioni wakati wenyeji Uganda watacheza na Ethiopia saa 1:00 usiku.Katika mechi za jana, Bara iliilaza Burundi mabao 7-0 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Lugogo mjini hapa. Matokeo hayo yanaifanya Bara itimize pointi sita baada ya kucheza mechi tatu na sasa, wakishinda mbili na kufungwa moja.Burundi imemalizaa kileleni mwa Kundi B, kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Sudan, bao pekee la Chris Nduwarugira jana. Rwanda iliifunga Eritrea 2-0, mabao ya Tadi Etikiama na Tumaine Ntamuhanga, huku Malawi ikiilaza Zanzibar 2-0.
ROBO FAINALIDesemba 3, 2012Tanzania Vs Rwanda Saa 8:00 mchana LugogoZanzibar Vs Burundi Saa 10:00 jioni LugogoDesemba 4, 2012Kenya Vs Malawi Saa 10:00 jioni NambooleUganda Vs Ethiopia Saa 1:00 usiku Namboole
VIWANGO VYA UBORA FIFANCHI NAFASIUganda 86Malawi 101Ethiopia 102Sudan 102Rwanda 122Burundi 128Kenya 130Tanzania 134Zanzibar 134Somalia 193Eritrea 192Sudan Kusini 200(Viwango hivi vimetoka mwezi huu)



MFUNGAJI bora wa Ligi Kuu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Taddy Etikiama amewaambia Yanga SC ya Dar es Salaam, wasikosee kusajili mshambuliaji mwingine yeyote zaidi yake, kwani yeye ndiye mkali anayewafaa zaidi.Akizungumza na fzakar jana mijini hapa, Taddy anayechezea Rwanda katika Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge alisema kwamba huu ni wakati mzuri Yanga kumsajili, kwani amemaliza mkataba na klabu yake A.S. Vita ya DRC.Alisema anaijua Yanga vizuri na mfumo wake wa uchezaji pia na anaamini akijiunga nayo atawafungia sana mabao. “Najua wana wapinzani wao wakubwa, Simba, mimi nikisajiliwa Yanga nitakuwa nawafunga sana hao Simba,”alisema Etikiama na kuongeza.“Mimi ni mkali kweli, nimekuwa mfungaji bora wa Kongo (DRC), nimefunga mabao 15 ligi yenye timu nzuri kama TP Mazembe, St Eloi Lupopo na DC Motema Pembe, nimewashinda akina Mbwana Samatta, Yanga wakinipata watapata mchezaji mzuri wa ushindi,”alisema.Taddy alikuwa na A.S. Vita kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, ambayo Yanga iliibuka bingwa.Katika mashindano hayo yaliyofanyika mjini Dar es Salaam Taddy alikaribia kuwa mfungaji bora baada ya kushika nafasi ya pili kwa mabao yake sita, nyuma ya Said Bahanuzi wa Yanga aliyefunga saba na kutwaa kaitu cha dhahabu cha michuano hiyo.Taddy alifunga idadi sawa ya mabao na mshambuliaji mwingine wa Yanga, Hamisi Kiiza ‘Diego‘, ambaye katika Challenge hii naye anachezea nchi yake, Uganda.   

Saturday, December 1, 2012


TANZANIA-TAIFA STARS.
KIKOSI CHA TANZANIA-TAIFA STARS .
MCHEZAJI WA TAIFA STARS AKIMTOKA MCHEZAJI WA SOMALIA HAPA.
STARIKA WA TIMU YA TAIFASTARS AKIONDOKA NAMPIRA .
MCHEZAJI WATAIFA STARS AKIRUKA KICHWA MPIRA WA JUU ZAIDI AKITOA PASS YA JUU.
KAPOMBE AKITOA PASS HAPA.
JOHN BOCCO AKIWATOKA WACHEZAJI  WA SOMALIA WAWILI HAPO.
MRISHO KHALFAN NGASSA AKIPOKEA PASS YA  JOHN BOCCO.
HATARI LANGONI MWA SOMALIA....
MRISHO KHALFAN NGASSA AKISHANGILIA GOLI LAKE HAPA.
MCHEZAJI WATIMU YA TAIFA WAKIMPONGEZA HAPO.
NGASSA ALIKUA ANAFURAHA KWELI HAPO.
MASHABIKI WA TIMU YA STARS WAKISHANGILIA  KWA RAHA ZAO.
MCHEZAJI WA TAIFA STARS AKIWATOKA WACHEZAJI WA SOMALI WOTE WAWILI
JOHN BOCCO AKIMBURUZA MCHEZAJI WA SOMALIA.
JOHN BOCCO YUPO KATIKA  HATARI LANGONI MWA SOMALIA.
HAYA SASA GOLI LA JOHN BOCCO AKISHANGILIA NA WACHEZAJI WENZAKE HAPO.
AKISHANGILIA KWA MARA YA MWISHO JOHN BOCCO.
DAKIKA ZAHATARI  MCHEZAJI MWENYE JEZI NO.5 AKIJARIBU KWENDA KUFUNGA GOLI LA 8
MPIRA  UMEKWISHA HAPA.
SHABIKI WATAIFA STARS ANAMADOIDO KWELI KWELI.

MRISHO Ngassa alifunga magoli matano peke yake na John Bocco 'Adebayor' akaongeza mengine mawili wakati timu ya taifa ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) ilipotoa kipigo kikubwa zaidi cha michuano ya Kombe la Chalenji la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati kwa mwaka huu cha magoli 7-0 dhidi ya Somalia katika mechi yao ya mwisho ya Kundi B kwenye Uwanja wa Lugogo, Kampala Uganda leo.
Kipigo cha 7-0 leo, kinarejea matokeo ya 7-0 ambayo Tanzania Bara iliifunga Somalia miaka 7 iliyopita (Desemba 2005) katika michuano hiyo.
Pamoja na kulipa kisasi baada ya Tanzania kufungwa na Somalia 1-0 mwaka jana, ushindi wa leo pia umeipeleka Kili Stars katika robo fainali ya Kombe la Chalenji ikiwa na pointi 6  katika nafasi ya pili ya Kundi B.
Burundi wamemaliza wakiwa vinara wa kundi hilo baada ya kushinda mechi yao ya tatu leo dhidi ya Sudan na kumaliza wakiwa na pointi 9.
Sudan ni wa tatu wakiwa na pointi 3 na watasubiri kuona kama wanaweza kusonga mbele kama 'Best Loosers', lakini Somalia ambao hawajaambulia hata pointi moja watafungasha virago kurejea makwao.
Magoli matano ya leo yanamfanya Ngassa kuwa kinara wa ufungaji katika michuano ya mwaka huu, akifuatiwa na Bocco, ambaye ana ma goli manne baada ya kufunga mawili pia katika mechi ya ufunguzi ambayo Kili Stars walishinda 2-0.
Ngassa alionekana kusahau kwamba anapaswa kuondoka na mpira kwa kufunga 'hat-trick' na alitumia muda wa baada ya firimbi ya mwisho kusalimia mashabiki wachache wa Tanzania waliokuwa pembeni ya uwanja kabla ya refa kumfuata na kumkabidhi mpira wake.
Zanzibar Heroes, Kenya, wenyeji Uganda wote pia wameshatinga hatua ya 8-Bora.