habari

MATANGAO

Sunday, December 2, 2012



MFUNGAJI bora wa Ligi Kuu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Taddy Etikiama amewaambia Yanga SC ya Dar es Salaam, wasikosee kusajili mshambuliaji mwingine yeyote zaidi yake, kwani yeye ndiye mkali anayewafaa zaidi.Akizungumza na fzakar jana mijini hapa, Taddy anayechezea Rwanda katika Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge alisema kwamba huu ni wakati mzuri Yanga kumsajili, kwani amemaliza mkataba na klabu yake A.S. Vita ya DRC.Alisema anaijua Yanga vizuri na mfumo wake wa uchezaji pia na anaamini akijiunga nayo atawafungia sana mabao. “Najua wana wapinzani wao wakubwa, Simba, mimi nikisajiliwa Yanga nitakuwa nawafunga sana hao Simba,”alisema Etikiama na kuongeza.“Mimi ni mkali kweli, nimekuwa mfungaji bora wa Kongo (DRC), nimefunga mabao 15 ligi yenye timu nzuri kama TP Mazembe, St Eloi Lupopo na DC Motema Pembe, nimewashinda akina Mbwana Samatta, Yanga wakinipata watapata mchezaji mzuri wa ushindi,”alisema.Taddy alikuwa na A.S. Vita kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, ambayo Yanga iliibuka bingwa.Katika mashindano hayo yaliyofanyika mjini Dar es Salaam Taddy alikaribia kuwa mfungaji bora baada ya kushika nafasi ya pili kwa mabao yake sita, nyuma ya Said Bahanuzi wa Yanga aliyefunga saba na kutwaa kaitu cha dhahabu cha michuano hiyo.Taddy alifunga idadi sawa ya mabao na mshambuliaji mwingine wa Yanga, Hamisi Kiiza ‘Diego‘, ambaye katika Challenge hii naye anachezea nchi yake, Uganda.   

No comments:

Post a Comment