habari

MATANGAO

Sunday, December 30, 2012



YANGA SC, mabingwa mara tano wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame wameondoka Alfajiri ya leo, saa 10:30 usiku kwenda Uturuki kuweka kambi ya mazoezi ya wiki mbili.
Kikosi kizima cha Yanga kilikuwa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere tangu saa 8:00 usiku kwa taratibu za kusafiri katika ziara hiyo ya kwanza nje ya Afrika tangu walipokwenda Brazil mwaka 1974.
Yanga itaweka kambi katika mji wa Antalya uliopo kusini mwa Uturuki na itafikia katika hoteli ya Sueno Beach iliyopo pembezoni mwa bahari ya Meditreanian, na itakua ikifanya mazoezi katika viwanja vikubwa viwili vilivyopo katika hotel hiyo na kiwanja kidogo cha nyasi bandia.
Kikosi cha Yanga kilichoondoka Alfajiri ya leo ni makipa; Ally Mustafa 'Barthez', Said Mohamed na Yussuf Abdul, mabeki Juma Abdul, Shadrack Nsajigwa, Godfrey Taita, Stefano Mwasyika, Oscar Joshua, Mbuyu Twite, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Ladisalus Mbogo na Kelvin Yondani.
Viungo ni Athumani Iddi ‘Chuji’, Frank Domayo, Haruna Niyonzima, Kabange Twite, Nurdin Bakari, Omega Seme, Simon Msuva, Rehani Kibingu, Nizar Khalfani na David Luhende wakati washambuliaji ni Didier Kavumbagu, Said Bahanunzi, Jerry Tegete, George Banda na Hamisi Kiiza.
Upande wa benchi la ufundi ni Kocha Mkuu Mholanzi, Ernie Brandts, Kocha Msaidizi Freddy Felix Minziro na Kocha wa makipa, Razak Ssiwa, na Maofisa wengine ni Daktari wa timu, Sufiani Juma, Meneja Hafidh Saleh, Ofisa Habari, Baraka Kizuguto Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Mohammed Nyenge.
Mwandishi wa Gazeti la Mwanaspoti, Michael Momburi yupo kwenye ziara hiyo ya kwanza ya Yanga Ulaya, yeye akigharamiwa na kampuni yake.
Ziara ya mwisho katika nchi ya maana kwa Yanga, ilikuwa mwaka 2008 nchini Afrika Kusini, ambako iliweka kambi ya zaidi ya wiki mbili wakati huo ikiwa chini ya Profesa Dusan Savo Kondic, raia wa Serbia.
Zaidi ya hapo, mwaka huu Yanga ilikwenda Kigali, Rwanda kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu ya Bara, kwa mwaliko wa rais wa nchi hiyo, Paul Kagame.
Yanga SC ni klabu kongwe Tanzania ambayo kati ya zinazoshiriki Ligi Kuu kwa sasa, yenyewe ndio yenye umri mkubwa zaidi.
Ingawa historia inasema Yanga ilizaliwa mwaka 1935 na Simba mwaka 1936, lakini ukizama ndani utagundua kwamba, huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa utani na upinzani wa jadi, baina ya miamba hiyo ya soka nchini.
Kulikuwa kuna timu inaitwa New Youngs, ambayo mwaka 1938 ilisambaratika na baadhi ya wachezaji wake wakaenda kuunda timu iliyokuwa ikiitwa Sunderland, ambayo hivi sasa inajulikana kama Simba.
Kabla ya kutokea vurugu zilizoisambaratisha New Youngs, vijana wa Dar es Salaam walikuwa wana desturi ya kukutana viwanja vya Jangwani kufanya mazoezi na baada ya muda wakaamua kuunda timu yao, waliyoipachika jina Jangwani.
Ndani ya kipindi kifupi tu, timu hiyo iliteka hisia za wengi, waliojitokeza kujiandikisha uanachama wa klabu hiyo. Miongoni mwa waliovutika na uanachama wa klabu hiyo ni Tarbu Mangara (sasa marehemu) na ilipofika mwaka 1926, walifanya mkutano wa kwanza katika eneo ambalo hivi kuna shule ya sekondari ya Tambaza.
Miongoni mwa yaliyojadiliwa kwenye mkutano huo ni kuiboresha timu hiyo, ambayo wachezaji wake wengi walikuwa wafanyakazi wa Bandarini na mashabiki wake wengi walikuwa wabeba mizigo wa bandarini.
Baada ya mkutano huo, timu hiyo ilibadilishwa jina na kuwa Navigation, iliyotokea kuwa moto wa kuotea mbali katika timu za Waafrika enzi hizo, kabla ya uhuru wa Tanganyika. Timu kama Kisutu, Kitumbini, Gerezani na Mtendeni zilikuwa hazifui dafu kwa wana Jangwani hao.
Ikiwa inatamba kwa jina la Navigation, wanachama wa timu hiyo walikuwa wakitembea kifua mbele na kuwatambia wapinzani, kwamba wao ndiyo zaidi. Kwa sababu katika kipindi hicho, Italia ilikuwa inatamba kwenye ulimwengu wa soka, wanachama wa timu hiyo nao waliamua kuibadilisha jina timu yao na kuiita Taliana.
Taliana ilipata mafanikio ya haraka na haikushangaza ilipopanda hadi Ligi Daraja la Pili Kanda ya Dar es Salaam, mwanzoni mwa miaka ya 1930. jina la Taliana waliamua kuachana nalo mapema, kabla ya kuingia kwenye ligi hiyo, hivyo wakaanza kujiita New Youngs.
Lakini kila ilipokuwa ikibadilisha jina, ilikuwa ikifanya vitu pia, kwani wakiwa na jina la New Youngs, waliweza kutwaa Kombe la Kassum, lililoshirikisha timu mbalimbali za  Dar es Salaam.
Hatimaye ukawadia mwaka mbaya kwa New Youngs, 1938 wakati baadhi ya wachezaji walipojitoa na kwenda kuanzisha Sunderland. Kwa sababu hiyo, waliobaki wakaamua kubadili jina na kuwa Young Africans, jina ambalo mashabiki wake wengi walishindwa kulitamka vizuri hivyo kujikuta wakisema Yanga. Safari njema Yanga SC.

Thursday, December 27, 2012


MABINGWA wa soka Tanzania Bara, Simba SC wamepangwa kundi moja, A na Tusker FC ya Kenya, Bandari ya Unguja na Jamhuri ya Pemba katika michuano ya Kombe la Mapinduzi, inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi hivi karibuni visiwani Zanzibar.
Aidha, katika Kundi B, washindi wa pili wa Ligi Kuu ya Bara, Azam FC ya Dar e Salaam pia, imepangwa na Mtibwa Sugar ya Morogoro, Coastal Union ya Tanga na Miembeni ya Unguja.
Michuano ya Kombe la Mapinduzi, ambayo ni maalum kwa ajili ya kuherehekea Mapinduzi matukufu ya Zanzaibar, inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Januari 2, hadi kilele cha miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Januari 12, mwakani, huku ikishirikisha timu kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Kwa mujibu wa ratiba ya michuano hiyo iliyotolewa na Kamati Maalum ya Kusimamaia michuano hiyo, inaonesha kuwa katika mchezo wa kwanza utakaochezwa siku ya ufunguzi itakuwa ni kati ya Bandari kutoka Unguja ambayo itacheza na Jamhuri kutoka kisiwani Pemba ambao ni wawakilishi wa Zanzibar katika Kombe la Shirikisho Barani Afrika, pamabano litakalochezwa katika uwanja wa Mao Tse Tung mjini Unguja, huku usiku wa siku hiyo hiyo katika Uwanja wa Amaan kisiwani Unguja pambano la ufunguzi rasmi katika mashindano hayo likiwakutanisha mabingwa wa soka nchini Tanzania, Simba SC ambao watapambana na mabingwa wa soka nchini Kenya, Tusker.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo jumla ya timu nane zitashiriki katika mashindano hayo ambayo yamejipatia umaarufu mkubwa visiwani hapa, timu hizo zimegawanya katika makundi mawili ambayo ni kama ifuatavyo:
Awali michuano hiyo ilitarajiwa kuanza kisiwani Pemba tarehe 1 Januari, lakini kutokana na kujitoa katika mashindano kwa klabu ya Al-Ahly ya Misri kutokana na klie kilichoelezwa sababu za kiusalama, mechi zote sasa zitachezwa kisiwani Unguja na ufunguzi ukipangwa kuanza tarehe 2 badala ya tarehe 1 januari.
Bingwa wa michuano hiyo ataondoka na zawadi ya kombe na fedha taslim Tsh. Milioni kumi (10,000,000), mshindi wa pili Milioni tano (5,000,000), pamoja na zawadi nyengine ambazo zimegawanywa katika makundi tofauti ikiwemo zawadi ya mfungaji bora, mchezaji bora, mwamuzi bora, kipa bora, mwandishi wa habari bora, timu bora na zawadi nyeanginezo.
Kupitia matandao wako makini wa http://bongostaz.blogspot.com/ tutakuwa ukiwaletea kila kitakachoendelea katika mashindano hayo kuanzia mwanzo mpaka mwisho

Wednesday, December 26, 2012


MABINGWA wa Kenya, Tusker FC jioni hii wameiangusha Yanga SC bao 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kirafiki jioni hii.
Huo ulikuwa mchezo maalum kwa Yanga kuwaaga mashabiki wake, kabla ya safari ya Uturuki Jumamosi usiku kwenda kuweka kambi ya wiki mbili.
Wachezaji wa Tusker wakimpongeza mfungaji wa bao lao,
Ismail Dunga kulia
Hadi mapumziko, Tusker walikuwa tayari mbele kwa bao hilo 1-0, lililowekwa kimiani na kiungo Ismail Dunga kwa mkwaju wa penalti dakika ya 44.
Refa Charles Oden Mbaga alitoa penalti hiyo baada ya kiungo wa Yanga, Nurdin Bakari kumuangusha kwenye eneo la hatari, kiungo Khalid Aucho.
Yanga walicheza vema katika kipindi hicho, lakini hawakufanikiwa kutengeneza nafasi za  kufunga na hilo lilitokana na mipango haba ya safu yake ya kiungo leo, ikiongozwa na Kabange Twite na Nurdin Bakari.
Pamoja na kocha Mholanzi Ernie Brandts kufanya mabadiliko kipindi cha pili, akiwaingiza Hamisi Kiiza, Jery Tegete, Simon Msuva, Omega Seme na Nizar Khalfan kuchukuwa nafasi za akina David Luhende, Said Bahanuzi, George Banda, Rehani Kibingu na Oscar Joshua, lakini matokeo hayakubadilika.
Zaidi Yanga iliongeza kasi ya mashambulizi kupitia kwa Msuva na Kiiza na hata Nizar alipoingia, lakini kwa ujumla bahati haikuwa yao jioni ya leo.
Hii ni mechi ya pili Brandts anafungwa kati ya mechi 10 alizoiongoza Yanga tangu aanze kazi akirithi mikoba ya Mbelgiji, Tom Saintfiet, nyingine saba ameshinda na moja ametoa sare.
Yanga SC; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Ladislaus Mbogo, Nurdin Bakari, Rehani Kibingu, Kabange Twite, George Banda, Said Bahanuzi na David Luhende.
Tusker FC; George Opiyo, Luke Ochieng, Jeremiah Bright, Mark Odhiambo, Joseph Shikokoti, Khalid Aucho, Edwin Manono, Justin Monda, Ismail Dunga, Jesse Were, Robert Omonuk,  

Sunday, December 23, 2012


azam fc-football club leo ime fanikiwa kuchukuwa ubingwa wa hisani ya DRC 2012/2013,katika uwanja wa drc wakiwa na shangwe la kombe lao.

Saturday, December 22, 2012

TAZAMENI PICHAZA,TANZANIA-TAIFA STARS VS ZAMBIA-CHIPOLOPOLO LEO KATIKA UWANJA WA DAR-ES-SALAAM.
KIKOSI CHA TAIFA STARS-TANZANIA.
KIKOSI CHA ZAMBIA -CHIPOLOPOLO.
UBAO WA MATOKE UKIONESHA TANZANIA1-ZAMBIA 0.
MCHEZAJI WA TANZANIA AKIUWAHI MPIRA MBELE AKIWA MCHEZAJIWA ZAMBIA..
HATARI LANGONI MWAZAMBIA,MCHEZAJI WA TAIFA STARS AKIJARIBU KUUPIGA MPIRA,MABEKI WA TATU WA KIMZUNGUKA..
MASHABIKI WA ZAMBIA WAKIISHANGILIA TIMU YAO.
MCHEZAJI WA TAIFA STARS AKIJARIBU KUWATOKA WACHEZAJI WA ZAMBIA,WACHEZAJI WA ZAMBIA WAMEMKATALIA....
MCHEZAJI WA ZAMBIA AKIJARIBU KUUWOKOA,NA AKATELEZA NAO..
MASHABIKI WATAIFA  STARS NI FULL SHANGWE TU.
KABLA YA MECHI MAWAZIRI WAZAMBIA WAKIWASALIMIA WATANZANIA...
HATARI LA NGONI MWA ZAMBIA TENA.....
HAPA NI  FURAHA KWELI KWELI...........
MASHABIKI WAKIMSHANGILIA MCHEZAJI MRISHO NGASA KWA KUIFUNGA ZAMBIA 1-0
HATARI MRISHO KHALFAN NGASA....
MRISHO KHALFAN NGASA AKISHANGILIA GOLI LAKE NA WA CHEZAJI WA TAIFASTARS..
KOCHA WA TIMU YA TAIFA STARS AKIMUAMBIA KOCHA WA ZAMBIA,YOUR TEAM IS HAVING BAD DEFENDER...
MPIRA UMEISHA WACHEZAJI WAKIONDOKA UWANJANI......






KAMA ingekuwa ni ndondi, leo Tanzania wangetawazwa kuwa mabingwa wapya wa Afrika, baada ya kuwapiga Zambia, lakini katika soka, haiku hivyo.
Tanzania, Taifa Stars leo imeendeleza wimbi lake la ushindi katika michezo ya kirafiki baada ya kuifunga Zambia 1-0, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika mchezo wa leo, hadi mapumziko, tayari Stars ambayo Novemba 14, mwaka huu iliifunga 1-0 Kenya, Uwanja wa CCM Kirumba, walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililowekwa kimiani na kiungo mshambuliaji Mrisho Khalfan Ngassa.
Ngassa, anayecheza kwa mkopo Simba SC akitokea Azam FC, zote za Dar es Salaam, alifunga bao hilo dakika ya 45, akimalizia pasi nzuri ya kiungo wa Simba SC, Mwinyi Kazimoto.
Stars ilicheza vizuri na kwa umakini wa hali ya juu kipindi cha kwanza, na kufanikiwa kuwabana mabingwa hao wa Afrika wanaojiandaa kwenda kutetea taji lao nchini Afrika Kusini mapema mwakani.
Kipindi cha pili, Zambia walianza kwa kurekebisha kikosi chao, kocha Mfaransa, Herve Renard akiwatoa Hichani Himonde, Moses Phiri, Sinkala na Isaac Chansa na nafasi zao  kuchukuliwa na Stopila Sunzu, Mukuka Mulenga, Evans Kangwa na Francis Kasonde.
Pamoja na mabadiliko hayo, Stars iliendelea kung’ara na katika dakika ya 57 Ngassa alikaribia kufunga tena kama si shuti lake kufuatia pasi ‘tamu sana’ ya Sure Boy kutoka nje.
Lakini kukosa kwa Ngassa bao hilo, kulitokana na maarifa ya beki wa TP Mazembe ya DRC, Stopila Sunzu anayejiandaa kuhamia Reading ya England, ambaye alimbana kiungo huyo wa Simba kumynima mwanya wa kupiga vizuri na akafanikiwa kumfanya apige nje.
Zambia walipoteza nafasi nzuri ya kusawazisha bao dakika ya 76, baada ya shuti la Chasamba Lungu kugonga mwamba, wakati kipa Juma Kaseja akiwa amekwishapotea maboya.
Ngassa alijibu shambulizi hilo dakika ya 77 baada ya shuti alilojaribu kupaa juu ya lango, huku Felix Katongo akipewa kadi ya njano, baada ya kumuangusha Amri Kiemba aliyekuwa anamfunga tela.
Juma Kaseja alifanya kazi ya ziada dakika ya 86, baada ya kuokoa shuti la karibu la Chris Katongo na katika dakika ya 87, Stars ilipata pigo baada ya beki Kevin Yondan kuumia na nafasi yake kuchukuliwa beki mwenzake wa Yanga, Nadir Haroub Ally ‘Cannavaro’ dakika ya 88.
Kikosi cha Stars leo kilikuwa; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, Aggrey Morris, Kevin Yondan/Nadir Haroub dk 87, Frank Domayo, Salum Abubakar, Mwinyi Kazimoto, Amri Kiemba, Mrisho Ngassa/Amir Maftah dk83 na Khamis Mcha ‘Vialli’/Simon Msuva dk59.
Zambia; Danny Munyao, Chintu Kampamba, Hichani Himonde, Chisamba Lungu, James Chamanga, Moses Phiri, Chris Katongo, Felix Katongom Nathan Sinkala/, Rodrick Kabwe na Isaac Chansa. 

Friday, December 21, 2012



AZAM FC imefanikiwa kutinga Fainali ya Kombe la Hisani, baada ya kuifunga kwa mikwaju ya penalti 5-4 Shark FC ya hapa, kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90 kwenye Uwanja wa Martyrs jioni hii.
Nahodha Jabir Aziz Stima ndiye aliyekwenda kupiga penalti ya mwisho, Shark wakitoka kupoteza, kufuatia mpira kugonga mwamba. Aiziz aliwainua vitini wachezaji wenzake na makocha wake pamoja na viongozi wa wachache wa timu hiyo waliopo hapa kwa kupiga penalti maridadi iliyotinga nyavuni.
Azam sasa, itamenyana na mshindi wa mechi inayoendelea hivi sasa kati ya Dragons na FC MK Jumapili katika fainali.
Azam iliuanza mchezo huo vizuri na ikicheza kwa maelewano makubwa sambamba na kushambulia kwa kasi kutokea pembeni, kulia Kipre Herman Tchetche na kushoto Seif Abdallah.
Hata hivyo, shambulizi la kushitukiza la Shark liliwapa bao la kuongoza dakika ya 16, lililofungwa na Ngulubi Kilua, baada ya mabeki wa Azam kudhani ameotea.
Iliwachukua dakika 10 tu Azam kusawazisha bao hilo, mfungaji akiwa Gaudence Exavery Mwaikimba aliyeunganisha kwa kichwa krosi maridadi ya nyota wa mchezo wa leo, Kipere Herman Tcheche kutoka wingi ya kulia.
Baada ya bao hilo, Azam iliendelea kuwashambulia Shark na dakika ya 37, Kipre Tchetche aliifungia timu hiyo bao la pili, kufuatia kazi nzuri ya Mwaikimba. Mwaikimba alipokea mpira mrefu, akatuliza na kumtangulizia kwa mbele mfungaji, ambaye hakufanya makosa, alimchambua kipa wa timu inayomilikiwa na mdogo wa rais wa DRC, Joseph Kabila.
Hadi mapumziko, Azam ilikuwa inaongoza kwa mabao 2-1 na kipindi cha pili Shark waliingia kwa kasi na kufanikiwa kusawazisha kwa penalti dakika ya 47, iliyotiwa nyavuni na Bukasa Kalambai, ambaye yeye mwenyewe alijiangusha kwenye eneo la hatari baada ya kuzongwa na beki David Mwantika.
Baada ya dakika 90 kutimu timu hizo zikiwa zimefungana 2-2, sheria ya matuta ilichukua mkondo wake na wachezaji wote watano wa Azam waliopewa dhamana hiyo leo na kocha Muingereza Stewart Hall, walitimiza wajibu wao vizuri.
Kipre Tchetche alifunga ya kwanza, Mwaikimba ya pili, Jaockins Atudo ya tatu, Himid Mao ya nne na Stima akapiga ya ushindi.
Stewart alisema amefurahishwa na matokeo ya mchezo wa leo na sasa ana matumaini ya timu yake kurejea na Kombe hilo Dar es Salaam.
Katika mchezo wa leo, kikosi cha Azam kilikuwa; Mwadini Ally, Himid Mao, Samih Hajji Nuhu, Joackins Atudo, David Mwantika, Jabir Aziz, Kipre Balou, Seif Abdallah/Uhuru Suleiman dk 77, Kipre Tchetche, Humphrey Mieno na Gaudence  Mwaikimba.  



PICHA ZA, AZAM FC-FOOTBALL CLUB WAKISHANGILIA ,KUINGIA FAINALI....

PICHA ZA, AZAM FC-FOOTBALL CLUB WAKISHANGILIA ,KUINGIA FAINALI....

Thursday, December 20, 2012

mchezaji wa Rwanda anaye fahamika kwa jina kama HAMISI KIIIZA DIEGO leo kasha enda makao makuu ya yanga sport club ya tanzania, baada ya mapumziko  ya cecafa  amerejea na timu yake yanga sport club...

Wednesday, December 19, 2012


AZAM FC imefanikiwa kuingia Nusu Fainali ya Kombe la Hisani mjini hapa, baada ya kuilaza Real de Kinshasa kwenye Uwanja wa Martyrs, katika mchezo maalum wa kutafuta timu ya kutinga Nusu ya michuano hiyo inayoandaliwa na FECOFA, Shirikisho la Soka DRC.
Shukrani kwao, washambuliaji Gaudence Mwaikimba na Seif Abdallah waliofunga mabao hayo, moja kila kipindi.
Ikiongezewa nguvu na nyota wake watatu, Kipre Tchetche, Kipre Balou raia wa Ivory Coast na Mkenya, Joackins Atudo waliochelewa mechi mbili za awali, Azam leo ilitawala mchezo na kama si rafu za wapinzani wao, ingevuna ushindi mtamu.
Hadi mapumziko, tayari Azam walikuwa mbele kwa bao 1-0, lililotiwa kimiani na Mwaikimba dakika ya 21, ambaye aliunganisha pasi nzuri ya Kipre kutoka wingi ya kushoto.
Hilo linakuwa bao la pili kwa Mwaikimba, mshambuliaji wa zamani wa Kahama United, Ashanti United, Yanga, Prisons na Kagera Sugar katika mechi tatu za mashindano haya alizocheza, awali alifunga katika sare ya 1-1 na Dragons.
Kipre Tchetche alilazimika kutoka nje ya Uwanja dakika ya 43 kutokana na rafu za wachezaji wa Real, nafasi yake ikichukuliwa na Samih Hajji Nuhu.
Real walikuwa wakipiga kiatu haswa na kiungo Waziri Salum aliungana na Kipre Tchetche kuuacha Uwanja kabla ya filimbi ya kuugawa mchezo, ingawa nafasi yake ilichukuliwa na Uhuru Suleiman dakika ya kwanza ya kipindi cha pili.
Awali ya hapo, refa Madila Achille alimtoa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 43 beki Muipalayi Igongo kwa kumchezea rafu mbaya Gaudence Mwaikimba, ambayo chupuchupu naye imtoe nje, kiasi cha kulazimika kumalizia mechi akichechemea.
Kipindi cha pili, Azam waliendelea kuwafundisha soka Real na katika dakika ya 73, kazi nzuri ya Mwaikimba ilisaidia kupatikana bao la pili. Mpira mrefu uliopigwa na kipa Mwadini Ally, Mwaikimba aliumiliki vema, akatoa pasi pembeni kushoto kwa Hajji Nuhu ambaye aliingia ndani kidogo na kukata krosi maridadi iliyounganishwa kimiani na Seif.
Humphrey Mieno alikuwa mwathirika mwingine wa rafu za Real, baada ya kulazimika kutoka nje dakika ya 77, akimpisha Abdi Kassim ‘Babbi’.
Azam walionekana kuridhika baada ya kuwa wanaongoza mabao 2-0 na wakafanya uzembe uliowapa bao la kufutia machozi Real, lililofungwa na Bisole Panzu dakika ya 78.
Baada ya mechi hiyo, kocha wa Azam, Muingereza Stewart Hall aliwapongeza vijana wake, lakini akasema anakabiliwa na wakati mgumu katika hatua inayofuata kutokana na wachezaji wake wanne kuumia leo.
Kocha wa Real, Sandra Makombele aliwasifu Azam ni timu nzuri na akasema anakubali matokeo, ingawa aliwapiga kijembe. “Wachezaji wangu wana mazoezi mengi, Azam hawana mazeozi, wakiguswa kidogo wanaumia, hakukuwa na rafu, ule ni mchezo wa nguvu kama Ulaya, kocha wao inabidi awape mazoezi mengi wawe wagumu,”alisema mwanamama huyo.
Katika mechi zake mbili za awali za Kundi B, Azam ilitoka 1-1 na Dragons na ikafungwa 2-0 na Shark FC.
Azam ilicheza mechi zote mbili bila makocha wake wote wawili, Waingereza Stewart Hall na Msaidizi wake, Kali Ongala ambao walibaki Nairobi, Kenya pamoja na Daktari Mjerumani Paulo Gomez na wachezaji Kipre Balou na Kipre Tcheche raia wa Ivory Coast, kutokana na kukosa viza za kuingia DRC.
Watano hao, waliwasili mjini Kinshasa jana na beki Joackins Atudo naye amewasili leo na wote wameshiriiki mchezo wa leo kikamilifu.
Nusu Fainali zitachezwa Desemba 25 wakati Desemba 26 itakuwa Fainali na mechi ya kusaka mshindi wa tatu.
Kikosi cha Azam leo kilikuwa; Mwadini Ally, Himid Mao, Waziri Salum/Uhuru Suleiman dk46, Omar Mtaki/Joackins Atudo dk46, David Mwantika, Jabir Aziz, Kipre Balou/Malika Ndeule dk85, Seif Abdallah, Kipre Tchetche/Samih Hajji dk43, Humphrey Mieno/Abdi Kassim dk77 na Gaudence Mwaikimba.

Monday, December 17, 2012


SASA rasmi, Yaw Berko amebaki historia ndani ya klabu ya Yanga. Hiyo inafuatia klabu ya St Eloi Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuridhika naye baada ya majadribio.
Katibu wa Yanga, Lawrence Mwalusako ameiambia fzakar.blogspot.com jana kwamba kipa huyo Mghana amefuzu majaribio Lupopo na amesajiliwa moja kwa moja.
Kuondoka kwa Berko, kunatoa nafasi kwa kiungo kutoka DRC, Kabange Twite kusajiliwa katika klabu hiyo ya Jangwani, akiungana na kaka yake, beki Mbuyu Twite. Wachezaji wengine wa kigeni wa Yanga ni kiungo Haruna Niyonzima kutoka Rwanda na washambuliaji Didier Kavumbangu kutoka Burundi na Hamisi Kiiza kutoka Uganda.
Berko alijiunga na Yanga SC mwaka 2009, akitokea Liberty Proffessional ya kwao Ghana, timu ambayo ilimuibua pia Michael Essein na nyota wengine kibao wa Ghana. Aliletwa nchini na kocha wa zamani wa Yanga, Mserbia Kostadin Bozidar Papic aliyewahi kupiga kazi Ghana katika klabu ya Hearts POf Oak.
Alikuwa kipa bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Bara msimu wa 2010/2011 na katika kipindi chake cha kufanya kazi Jangwani, anajivunia kuiwezesha timu kutwaa mataji ya ubingwa wa Bara msimu wa 2010/2011 na Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame mara mbili mfululizo, 2011 na 2012.
2011 alidaka mechi zote, lakini 2012 alidaka hadi Robo Fainali alipoumia na kumuachia Ally Mustafa ‘Barthez’ aliyedaka hadi ubingwa. Yanga imeridhika na uwezo wa Barthez langoni iliyemsajili kutoka Simba msimu huu na kuamua kuachana na Berko, ambaye alikuwa kipenzi cha wapenzi wa klabu hiyo.
Awali, Yanga ilijifikiria mara mbili kuachana na Berko, kwa kuhofia Barthez angeanza ‘kuwaringia’ kwa kuona amebaki peke yake kipa bora, lakini imepanga kumhamasisha Said Mohamed kuimarisha kiwango chake, vinginevyo atatemwa mwishoni mwa msimu.
Na Yanga imekuwa na ‘jeuri’ ya kumtema Berko baada ya kuona mwakani haitashiriki michuano ya Afrika, zaidi ya Ligi Kuu na jukumu la kwenda kutetea taji lake la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame mjini Kigali, Rwanda.
Japokuwa anaondoka, lakini kwa uhodari wake langoni, Berko atabakia kwenye kumbukumbu ya mashabiki wa Yanga.

WASIFU WAKE:
JINA: Yaw Berko
KUZALIWA: Oktoba 13, 1980
ALIPOZALIWA: Accra, Ghana
KLABU ZA AWALI:
Mwaka Klabu
2000-2005: Liberty Professional
2005-2006: Pisico Binh Dịnh F.C. (Vietnam, mkopo)
2006-2009: Liberty Professional
2009- 2012: Yanga SC
2012: St Eloi Lupopo 

AZAM FC ya Dar es Salaam, imefungwa mabao 2-0 na Shark FC ya hapa, katika mchezo wake wa mwisho wa Kundi B, Kombe la Hisani, kwenye Uwanja wa Martyrs jioni hii.
Mabao ya washindi, timu inayomilikiwa na mdogo wake rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Joseph Kabila yalifungwa na Ndibu Kalala dakika ya 23 na Kalala Kabongo dakika ya 34.
Hata hivyo, kipigo hicho kimechangiwa kwa kiasi kikubwa na uchezeshaji mbovu wa marefa, ambao tangu mwanzo walionekana kuwapendelea wenyeji.
Azam leo imenyimwa penalti mbili za halali, moja kila kipindi, ya kwanza baada ya shuti la mshambuliaji Gaudence Mwaikimba kuzuiwa kwa mkono na beki wa Shark na ya pili kiungo Humphrey Mieno aliangushwa kwenye eneo la hatari, tena ndani ya sita akiwa amekwishamtoka kipa, lakini zote refa akapeta.
Washika vibendera nao walizima mashambulizi kadhaa ya Azam kwa kudai wachezaji walikuwa wameotea.
Mabao yote Azam walifungwa wakitoka kushambulia na hayakuwa na mushkeli, makosa ambayo walirekebisha na hawakuyarudia kipindi cha pili. Kipindi cha kwanza, timu zilishambuliana kwa zamu, lakini kipindi cha pili Azam walitawala zaidi mchezo na kama si ‘madudu’ ya refa, matokeo yangeweza kubadilika.
Kwa matokeo haya, Shark inaongoza Kundi B kwa pointi zake tatu, ikifuatiwa na Dragons iliyotoka 1-1 na Azam katika mchezo wa kwanza.
Azam sasa itaomba Shark iifunge zaidi ya mabao 2-0 Dragons katika mechi ya mwisho ya kundi hilo Desemba 23, ili ifuzu kuingia Nusu Fainali.
Azam imecheza mechi zote mbili bila makocha wake wote wawili, Waingereza Stewart Hall na Msaidizi wake, Kali Ongala ambao walibaki Nairobi, Kenya pamoja na Daktari Mjerumani Paulo Gomez na wachezaji Kipre Balou na Kipre Tcheche raia wa Ivory Coast, kutokana na kukosa viza za kuingia DRC.
Nusu Fainali zitachezwa Desemba 25 wakati Desemba 26 itakuwa Fainali na mechi ya kusaka mshindi wa tatu. Kundi B, lina timu za DC Motema Pembe, Diables Noirs, FC MK na Real De Kinshasa.
Kocha wa makipa, Iddi Abubakar aliyeiongoza timu hiyo katika mechi hizo mbili alilalamikia uchezeshaji wa marefa, ambao walisindikizwa na Polisi kutoka uwanjani baada ya mechi, kutokana na kuwakera hata mashabiki wa timu za hapa  waliotaka kuwafanyia fujo.
Kikosi cha Azam leo kilikuwa; Mwadini Ally, Malika Ndeule/Uhuru Suleiman dk 85, Samih Hajji Nuhu, Luckson Kakolaki/Omar Mtaki dk 65, David Mwantika, Jabir Aziz, Ibrahim Mwaipopo/Himid Mao dk80, Humphrey Mieno, Seif Abdallah, Gaudence Mwaikimba na Waziri Salum/Abdi Kassim ‘Babbi’ dk 65.

AZAM FC ya Dar es Salaam, imefungwa mabao 2-0 na Shark FC ya hapa, katika mchezo wake wa mwisho wa Kundi B, Kombe la Hisani, kwenye Uwanja wa Martyrs jioni hii.
Mabao ya washindi, timu inayomilikiwa na mdogo wake rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Joseph Kabila yalifungwa na Ndibu Kalala dakika ya 23 na Kalala Kabongo dakika ya 34.
Hata hivyo, kipigo hicho kimechangiwa kwa kiasi kikubwa na uchezeshaji mbovu wa marefa, ambao tangu mwanzo walionekana kuwapendelea wenyeji.
Azam leo imenyimwa penalti mbili za halali, moja kila kipindi, ya kwanza baada ya shuti la mshambuliaji Gaudence Mwaikimba kuzuiwa kwa mkono na beki wa Shark na ya pili kiungo Humphrey Mieno aliangushwa kwenye eneo la hatari, tena ndani ya sita akiwa amekwishamtoka kipa, lakini zote refa akapeta.
Washika vibendera nao walizima mashambulizi kadhaa ya Azam kwa kudai wachezaji walikuwa wameotea.
Mabao yote Azam walifungwa wakitoka kushambulia na hayakuwa na mushkeli, makosa ambayo walirekebisha na hawakuyarudia kipindi cha pili. Kipindi cha kwanza, timu zilishambuliana kwa zamu, lakini kipindi cha pili Azam walitawala zaidi mchezo na kama si ‘madudu’ ya refa, matokeo yangeweza kubadilika.
Kwa matokeo haya, Shark inaongoza Kundi B kwa pointi zake tatu, ikifuatiwa na Dragons iliyotoka 1-1 na Azam katika mchezo wa kwanza.
Azam sasa itaomba Shark iifunge zaidi ya mabao 2-0 Dragons katika mechi ya mwisho ya kundi hilo Desemba 23, ili ifuzu kuingia Nusu Fainali.
Azam imecheza mechi zote mbili bila makocha wake wote wawili, Waingereza Stewart Hall na Msaidizi wake, Kali Ongala ambao walibaki Nairobi, Kenya pamoja na Daktari Mjerumani Paulo Gomez na wachezaji Kipre Balou na Kipre Tcheche raia wa Ivory Coast, kutokana na kukosa viza za kuingia DRC.
Nusu Fainali zitachezwa Desemba 25 wakati Desemba 26 itakuwa Fainali na mechi ya kusaka mshindi wa tatu. Kundi B, lina timu za DC Motema Pembe, Diables Noirs, FC MK na Real De Kinshasa.
Kocha wa makipa, Iddi Abubakar aliyeiongoza timu hiyo katika mechi hizo mbili alilalamikia uchezeshaji wa marefa, ambao walisindikizwa na Polisi kutoka uwanjani baada ya mechi, kutokana na kuwakera hata mashabiki wa timu za hapa  waliotaka kuwafanyia fujo.
Kikosi cha Azam leo kilikuwa; Mwadini Ally, Malika Ndeule/Uhuru Suleiman dk 85, Samih Hajji Nuhu, Luckson Kakolaki/Omar Mtaki dk 65, David Mwantika, Jabir Aziz, Ibrahim Mwaipopo/Himid Mao dk80, Humphrey Mieno, Seif Abdallah, Gaudence Mwaikimba na Waziri Salum/Abdi Kassim ‘Babbi’ dk 65.

TIMU sita zimeshakata tiketi ya kucheza hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Uhai inayoshirikisha wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 (U20) wa klabu za Ligi Kuu ya Tanzania.

Hatua ya robo fainali ya michuano hiyo inayofanyika viwanja vya Karume na Chamazi, Dar es Salaam na kudhaminiwa na kampuni ya Said Salim Bakhresa kupitai maji Uhai itafanyika Desemba 19 mwaka huu kwenye viwanja hivyo hivyo.

Timu zilizofuzu kutoka kundi A ni Coastal Union ya Tanga, Mtibwa Sugar ya Morogoro na JKT Ruvu ya Dar es Salaam. Kundi C ni Oljoro JKT ya Arusha na Ruvu Shooting ya Pwani wakati iliyofuzu kutoka kundi A hadi sasa ni Azam pekee.

Katika mechi zilizochezwa leo asubuhi (Desemba 17 mwaka huu) Coastal Union na Mtibwa Sugar zimetoka suluhu kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, wakati Uwanja wa Azam ulishuhudia African Lyon ikiifunga Mgambo Shooting mabao 2-1.

Nafasi mbili za robo fainali zilizobaki kutoka kundi B zinawaniwa na timu za Simba, African Lyon na Polisi Morogoro. Mechi itakayochezwa leo saa 10 jioni katika Uwanja wa Chamazi kati ya Polisi Morogoro na Simba ndiyo itakayoamua timu zitakazoungana na Azam kutoka kundi hilo.


RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amewashukuru wajumbe wa Mkutano Mkuu kwa kupigia kura waraka wa marekebisho ya Katiba, kwani wametimiza wajibu wao.

Akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, Rais Tenga amesema marekebisho ya Katiba ni jambo muhimu, lakini lazima yapate ridhaa ya wanaohusika ambao ni wajumbe.

“Nawasukuru wajumbe kwa kupitisha jambo hili. Nawashukuru wote, waliokubali na waliokataa. Ndivyo demokrasia ilivyo. Tulitaka waseme ndiyo au hapana, hivyo tulitarajia kupata majibu yoyote kati ya hayo mawili.

Marekebisho mengine yalikuwa ni maelekezo (directives) kutoka FIFA na CAF. Katiba yetu inasema tutatekeleza maagizo ya CAF na FIFA, lakini kwa misingi ya utawala bora tuliona ni lazima tupate ridhaa kutoka kwa wajumbe,” amesema.

Jumla ya wajumbe waliopiga kura kwa njia hiyo ya waraka ni 103 ambapo 70 waliunga mkono wakati waliokataa ni 33. Idadi hiyo ni asilimia 68 ya kura zote zilizopigwa, hivyo kupatikana theluthi mbili ya kura zilizopigwa ili kufanya marekebisho kikatiba.

Vipengele vilivyoingizwa katika marekebisho hayo ni ‘club licencing’ kama ilivyoagizwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Kamati ya Rufani ya Uchaguzi wa TFF kama ilivyoshauriwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na kuondoa nafasi ya Makamu wa Pili wa Rais.

Vilevile Kamati ya Utendaji itakutana Desemba 23 mwaka huu kufanya marekebisho ya Kanuni za Uchaguzi, kutokana na kupitishwa kwa marekebisho hayo ambayo yanaunda Kamati ya Rufani ya Uchaguzi wa TFF. Pia itachagua wajumbe wa Kamati ya Rufani ya TFF.

Mkutano Mkuu wa TFF ambapo pia utakuwa na ajenda ya uchaguzi utafanyika Februari 23 na 24 mwakani. Kwa mujibu wa Katiba ya TFF, wajumbe wanatakiwa kupewa taarifa ya Mkutano Mkuu siku 60 kabla.

Saturday, December 15, 2012


TIMU YA TANZANIA YA AZAM FC-FOOT BALL CLUB LEO IMEANZA NA SARE WAKIWA DRC-CONGO,WAKIFUNGANA 1-1.

TIMU YA TANZANIA YA AZAM FC-FOOT BALL CLUB LEO IMEANZA NA SARE WAKIWA DRC-CONGO,WAKIFUNGANA 1-1.