habari

MATANGAO

Tuesday, November 27, 2012


KENYA wako hatarini kupokonywa uenyeji wa Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge mwakani na badala yake wakapewa Rwanda.
Habari kutoka kwenye Mkutano wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) uliofanyika Ijumaa iliyopita, zimesema kwamba Rwanda wameambiwa wakae tayari kwa uenyeji wa michuano hiyo, iwapo Kenya itachemsha.
Habari zinasema Mwenyekiti wa Shirikiasho la Soka Kenya (FKF), Sam Nyamweya, awali alisema katika Mkutano Mkuu wa CECAFA kwenye hoteli ya Serena, kwamba Kenya tayari imekwishapata mfadhili wa mashindano hayo.
Kasha baadaye, Mwenyekiti wa Shirikisho la Soka Rwanda, FERWAFA, Celestin Ntagungira, akasema itakuwa tayari kutaja jina la mdhmaini wa Challenge ndani ya wiki mbili wakipewa uenyeji.
Katika kuamua utata huo, Rais wa CECAFA Injinia Leodegar Tenga alisema haki za uenyeji wa Challenge ya mwakani zitakwenda kwa nchi ambayo kwanza itawahakikishia mdhamini wa mashindano.

No comments:

Post a Comment