habari

MATANGAO

Monday, November 26, 2012


KATIKA kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga ya Dar es Salaam inatarajia kwenda kuweka kambi ya wiki mbili nchini Uturuki mapema mwakani.Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Abdallah Ahmad Bin Kleb amesema leo katika Mkutano na Waandishi wa Habari, makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam kwamba ziara hiyo inatarajiwa kufanyika kati ya Desemba na Februari 25, mwakani.Alisema pendekezo la kambi hiyo lilitolewa na kocha mkuu wa Yanga, Mholanzi Ernie Brandts ambaye ana uzoefu na nchi hiyo ambayo ina vitu vinavyostahili kwa ajili ya timu kuweka kambi.Alisema ikiwa huko timu hiyo inatarajiwa kucheza mechi mbili za kitrafiki na timu zitkazotajwa baadaye.Aidha, kocha mkuu wa timu hiyo amewapandisha wachezaji watatu wa kikosi cha vijana chini ya  miaka 20 wakiwemo kipa, Yussuf Abdallah, George Banda na Rehan Kibinga.Katika hatua nyingine, Bin Kleb aliasema wanajivunia uongozi wa sasa chini ya Mwenyekiti, Alhaj Yussuf Manji, kwani timu imekuwa na mafanikio makubwa ikiwemo kutwaa kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kagame, kufanya vema katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ambao ulimalizika kwa timu  kuongoza.Alisema kufanya vizuri katika Ligi Kuu, ni matunda ya timu hiyo kuweka kambi nchini Rwanda baada ya Kombe la Kagame

No comments:

Post a Comment