habari

MATANGAO

Sunday, January 27, 2013


Taarifa ya michezo kutoka Tanzania Dar-es-salaam,leo Young African Sport Club ime endelea na ubabe wake wa magoli hatari sana katika u wanja wa Dar-es-salaam  young african sport club imeshinda magoli 3-1leo hii,magoli hayo ya kifungwa na Jerry Tegete na Simon Msuva,tazameni picha hapo chini........
Taarifa ya michezo kutoka Tanzania Dar-es-salaam,leo Young African Sport Club ime endelea na ubabe wake wa magoli hatari sana katika u wanja wa Dar-es-salaam  young african sport club imeshinda magoli 3-1leo hii,magoli hayo ya kifungwa na Jerry Tegete na Simon Msuva,tazameni picha hapo chini........

Saturday, January 26, 2013


SIMBA SC leo imeanza vyema mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kuichapa mabao 3-1 African Lyon ya Dar es Salaam katika mchezo wa ufunguzi wa duru hilo.
SIMBA SC leo imeanza vyema mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kuichapa mabao 3-1 African Lyon ya Dar es Salaam katika mchezo wa ufunguzi wa duru hilo.


SIMBA SC leo imeanza vyema mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kuichapa mabao 3-1 African Lyon ya Dar es Salaam katika mchezo wa ufunguzi wa duru hilo.
Ushindi huo, unaifanya
Hadi mapumziko Simba SC walioweka kambi ya wiki mbili Oman kujiandaa na mzunguko huu, tayari walikuwa mbele kwa mabao 3-0, yaliyotiwa kimiani na Mrisho Khalfan Ngassa mawili dakika za 19 na 39 na Ramadhan Suleiman Chombo ‘Redondo’ dakika ya tatu ya mchezo huo.
Redondo aliifungia Simba SC bao la kwanza dakika ya tatu, akiunganisha krosi nzuri ya Ngassa kutoka wingi ya kushoto na kufumua shuti akiwa katikati ya msitu wa mabeki wa Lyon.
Bao hilo liliwatia chaji Simba SC na kuanza kucheza soka maridadi zaidi, wakionana kwa pasi za mitindo yote, ndefu, fupi, za juu, chini hadi visigino na haikushangaza dakika ya 19 walipopata bao la pili.
Ilikuwa ni kazi nzuri ya Ngassa mwenyewe, ambaye baada ya kupata pasi ya Mwinyi Kazimoto Mwitula aliitoka ngome ya Lyon kabla ya kumchambnua kipa wa timu hiyo, Abdul Seif.
Baada ya kufunga bao hilo, Ngassa alikwenda moja kwa moja kwenye benchi la wachezaji wa akiba na kukumbatiana na Haruna Moshi Shaaban ‘Boban’ kisha kuwapa mikono wachezaji kadhaa na kurejea uwanjani.
Lyon walipoteza nafasi nzuri ya kupata bao dakika ya 31, baada ya Shamte Ally Kilalile kukosa penalti.
Refa Israel Mujuni alitoa penalti hiyo baada ya beki Paul Ngalema kumkwatua beki Fred Lewis aliyepanda kusaidia mashambulizi, hata hivyo mkwaju wa kwanza wa Shamte ulipanguliwa na Nahodha wa Simba, Juma Kaseja, lakini mwamuzi akaamuru irudiwe kwa madai kipa huyo alitokea kabla ya mpira kupigwa na safari hiyo mpigaji akapiga nje kabisa. 
Simba iliongeza kasi ya mashambulizi ikitumia mipira ya pembeni, kulia akiteleza Chanongo na kushoto Ngassa, timu ikichezeshwa vyema na viungo watatu katikati, Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto na Jonas Mkude. Ilikuwa burudani kwa mashabiki wa Wekundu hao wa Msimbazi, kwa jinsi ambayo timu yao ilitawala mchezo.
Kazi nzuri ya Chanongo aliyeteleza wingi ya kulia huku akiruka madaluga ya mabeki wa Lyon, iliipatia Simba bao la tatu baada ya krosi yake nzuri kuunganishwa vyema kimiani na Ngassa.
Baada ya kufunga, Ngassa alishangilia kwa aina yake bao hilo, kwanza akitambaa hadi langoni na kisha kujilaza kwenye nyavu kubwa kama yeye ndio mpira.
Baada ya hapo, aliinuka na moja kwa moja kwenda tena kwenye benchi la wachezaji wa akiba akianza kushangilia na Boban, baadaye wachezaji wengine na kocha Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, ambaye alitumia kama sekunde 30 akizungumza naye jambo.
Kipindi cha pili, Lyon walibadilika na kuwabana Simba SC wasiongeze mabao zaidi, huku wao wakifanikiwa kupata bao la kufutia machozi, lililofungwa na Bright Ike dakika ya 59, pasi ya Fred Lewis.
Katika mechi nyingine, Mtibwa Sugar ililala 1-0 nyumbani mbele ya Polisi Morogoro, bao pekee la Muzamil Said dakika ya 76, Coastal Union iliifunga Mgambo JKT 3-1, Ruvu Shooting iliilaza 1-0 JKT Ruvu, bao pekee la Abdulrahman Seif dakika ya 90 Azam FC imeshinda 3-1 dhidi ya Kagera Sugar na JKT Oljoro imeilaza 3-1 Toto Africans.
Ushindi wa Azam ulitokana na mabao ya Abdi Kassim ‘Babbi’ dakika ya 20 na Khamis Mcha dakika za 31 na 66, wakati la Kagera lilifungwa na Paul Ngway dakika ya 82 na sasa timu hiyo imejiimarisha katika nafasi ya pili kwa kutimzia pointi 27, sasa ikizidiwa mbili tu Yanga iliyo kileleni.
Uwanja wa Mkwakwani, Tanga mabao ya Coastal yalifungwa na Philip Mugenzi dakika ya 18, Daniel Lyanga dakika ya 78 na Joseph Mahundi dakika ya 81, wakati la Mgambo lilifungwa na Peter Mwalyanzi dakika ya 89.
Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha, mabao ya Oljoro yalifungwa na Hassan Isihaka dakika ya 15, Paul Nonga dakika ya 51 na 57, wakati la Toto lilifungwa na Selemani Kibuta dakika ya 73.
Ligi hiyo itaendelea kesho wakati vinara, Yanga SC watakapomenyana na TZ Prisons kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Simba SC; Juma Kaseja, Nassor Masoud ‘Chollo’, Paul Ngalema/Kiggi Makassy, Mussa Mudde/Komabil Keita, Shomary Kapombe, Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto, Haruna Chanongo, Mrisho Ngassa/Abdallah Seseme, Amri Kiemba na Ramadhan Chombo ‘Redondo’.
African Lyon; Abdul Seif, Fred Lewis, Jacob Massawe, Mohamed Samatta, Abdulaghan Gulam/Hood Mayanja, Yussuf Mlipili, Jackson Kanywa, Aman Kyata/Yussuf Mgwao, Job Ibrahim, Shamte Ally/Bright Ike na Juma Seif ‘Kijiko’.

MSIMAMO WA LIGI KUU YA VODACOM 2012/2103:
P W D L GF GA GD Pts
1 Yanga 13 9 2 2 25 10 15 29
2 Azam 14 8 3 3 20 12 8 27
3 Simba SC 14 7 5 2 23 12 11 26
4 Mtibwa Sugar 14 6 4 4 18 13 5 22
5 Coastal Union 14 7 4 3 19 15 4 25
6 Kagera Sugar 14 5 6 3 16 13 3 21
7 Ruvu Shooting 14 7 2 5 20 17 3 23
8 Mgambo JKT 14 5 2 7 11 16 -5 17
9 JKT Ruvu 14 4 3 7 13 21 -8 15
10 JKT Oljoro 14 5 5 5 16 17 -1 17
11 TZ Prisons 13 3 5 5 8 12 -4 14
12 Toto African 14 2 6 6 11 18 -7 12
13 African Lyon 14 2 3 9 10 23 -13 9
14 Polisi Moro 14 1 4 9 5 16 -11 7

MATOKEO KAMILI MECHI ZA LEO:
Mtibwa Sugar 0-1 Polisi Morogoro
Coastal Union 3-1 Mgambo JKT
Ruvu Shooting 1-0 JKT RUVU
Azam FC 3-1 Kagera Sugar
JKT Oljoro 3-1 Toto Africans
KESHO; Januari 27, 2013
Yanga SC Vs TZ Prisons

Friday, January 18, 2013


Simba Sport Club ya Tanzania leo huko oman i meshindwa kutambaa badala wafunge hizo tatu wamefungwa  wao 3-1 goli lililo fungwa na Haruna moshi boban,hangalia picha hizi,sio mbaya tumeshinda ugenini@Ramadhani Abubakri. blogspot.com
SimbaSport Club ya Tanzania leo huko oman i meshindwa kutambaa badala wafunge hizo tatu wamefungwa  wao 3-1 goli lililo fungwa na Haruna moshi boban,hangalia picha hizi,sio mbaya tumeshinda ugenini@Ramadhani Abubakri. blogspot.com