habari

MATANGAO

Friday, July 5, 2013

HIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Burundi kuchezesha mechi ya kwanza ya mchujo ya Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN) kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Uganda (The Cranes) itakayofanyika Jumamosi (Julai 13 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

HIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Burundi kuchezesha mechi ya kwanza ya mchujo ya Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN) kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Uganda (The Cranes) itakayofanyika Jumamosi (Julai 13 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Waamuzi hao ni Thierry Nkurunziza atakayepuliza filimbi wakati wasaidizi wake watakuwa Jean Claude Birumushahu na Pascal Ndimunzigo. Mwamuzi wa akiba (fourth official) ni pacifique Ndabihawenimana.
Kamishna wa mechi hiyo Gebreyesus Tesfaye kutoka Eritrea. Tesfaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Eritrea na mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Mashindano ya CHAN.
CAF pia imeteua Leslie Liunda wa Tanzania kuwa Kamisaa wa mechi kati ya Burundi na Sudan itakayochezwa jijini Bujumbura.
Mechi hiyo ya kwanza ya mchujo ya Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN) itafanyika keshokutwa (Julai 7 mwaka huu). Liunda anatarajia kuondoka leo usiku (Julai 5 mwaka huu) kwenda Bujumbura.
Wakati huo huo: Jjumla ya makocha wa mpira wa miguu na walimu 28 kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na shule za msingi na sekondari wameteuliwa kuhudhuria kozi ya FIFA 11 For Health inayoanza keshokutwa (Julai 7 mwaka huu) Homboro mkoani Dodoma.
Kozi hiyo itakayomalizika Julai 20 mwaka huu itakuwa chini ya ukufunzi wa Rogasian Kaijage ambaye pia ni Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya wanawake (Twiga Stars).
Washiriki ni Abdul Mikoroti (Shule ya Msingi Nzasa), Baltazar Kagimbo (Shule ya Msingi Tabata Jica), Baraka Baltazar (Shule ya Msingi Muhimbili), David Kivinge (Shule ya Msingi Temeke), Dismas Haonga (Tambaza Sekondari), Exuperus Kisaka (Shule ya Msingi Mavurunza) na Hadija Kambi (Shule ya Msingi Karume).
Hamis Chimgege (Shule ya Msingi Tusiime), Hobokela Kajigili (Shule ya Msingi Buguruni), Issack Mhanza (Shule ya Msingi Airwing), Job Ndugusa (Shule ya Msingi Upanga), John Sebabili (TFF), Lutta Rucharaba (Shule ya Msingi Montfort), Maua Rahidi (Shule ya Msingi Uhuru Wasichana), Michael Bundala (TFF) na Mussa Kapama (Shule ya Msingi Bunju ‘A’).
Priscus Silayo (Shule ya Msingi J.K. Nyerere), Peter Manyika (TFF), Rajabu Asserd (Shule ya Msingi Mtoni Kijichi), Raphael Matola (TFF), Raymond Rupia (St. Anne Maria Academy), Renatus Magolanga (Ulongoni Sekondari), Ruth Mahenge (Shule ya Msingi Chang’ombe), Said Pambaleo (TFF), Sebastian Nkoma (TFF), Titus Michael (TFF), Wane Mkisi (Jangwani Sekondari).