HIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Burundi kuchezesha mechi ya kwanza ya mchujo ya Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN) kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Uganda (The Cranes) itakayofanyika Jumamosi (Julai 13 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Waamuzi hao ni Thierry Nkurunziza atakayepuliza filimbi wakati wasaidizi wake watakuwa Jean Claude Birumushahu na Pascal Ndimunzigo. Mwamuzi wa akiba (fourth official) ni pacifique Ndabihawenimana.
Kamishna wa mechi hiyo Gebreyesus Tesfaye kutoka Eritrea. Tesfaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Eritrea na mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Mashindano ya CHAN.
CAF pia imeteua Leslie Liunda wa Tanzania kuwa Kamisaa wa mechi kati ya Burundi na Sudan itakayochezwa jijini Bujumbura.
Mechi hiyo ya kwanza ya mchujo ya Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN) itafanyika keshokutwa (Julai 7 mwaka huu). Liunda anatarajia kuondoka leo usiku (Julai 5 mwaka huu) kwenda Bujumbura.
Wakati huo huo: Jjumla ya makocha wa mpira wa miguu na walimu 28 kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na shule za msingi na sekondari wameteuliwa kuhudhuria kozi ya FIFA 11 For Health inayoanza keshokutwa (Julai 7 mwaka huu) Homboro mkoani Dodoma.
Kozi hiyo itakayomalizika Julai 20 mwaka huu itakuwa chini ya ukufunzi wa Rogasian Kaijage ambaye pia ni Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya wanawake (Twiga Stars).
Washiriki ni Abdul Mikoroti (Shule ya Msingi Nzasa), Baltazar Kagimbo (Shule ya Msingi Tabata Jica), Baraka Baltazar (Shule ya Msingi Muhimbili), David Kivinge (Shule ya Msingi Temeke), Dismas Haonga (Tambaza Sekondari), Exuperus Kisaka (Shule ya Msingi Mavurunza) na Hadija Kambi (Shule ya Msingi Karume).
Hamis Chimgege (Shule ya Msingi Tusiime), Hobokela Kajigili (Shule ya Msingi Buguruni), Issack Mhanza (Shule ya Msingi Airwing), Job Ndugusa (Shule ya Msingi Upanga), John Sebabili (TFF), Lutta Rucharaba (Shule ya Msingi Montfort), Maua Rahidi (Shule ya Msingi Uhuru Wasichana), Michael Bundala (TFF) na Mussa Kapama (Shule ya Msingi Bunju ‘A’).
Priscus Silayo (Shule ya Msingi J.K. Nyerere), Peter Manyika (TFF), Rajabu Asserd (Shule ya Msingi Mtoni Kijichi), Raphael Matola (TFF), Raymond Rupia (St. Anne Maria Academy), Renatus Magolanga (Ulongoni Sekondari), Ruth Mahenge (Shule ya Msingi Chang’ombe), Said Pambaleo (TFF), Sebastian Nkoma (TFF), Titus Michael (TFF), Wane Mkisi (Jangwani Sekondari).
Tanzania sports
Friday, July 5, 2013
Monday, May 6, 2013
Stars ipo tayari
TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imepangwa kundi A la michuano ya Kombe la COSAFA ambapo itacheza mechi yake ya kwanza Julai 6 mwaka huu jijini Lusaka, Zambia dhidi ya Shelisheli.
Upangaji ratiba (draw) wa mashindano hayo ulifanyika juzi (Mei 3 mwaka huu) jijini Lusaka ambapo timu nyingine zilizo na Taifa Stars katika kundi hilo ni Namibia na Mauritius. Kundi la Taifa Stars litachezea mechi zake jijini Lusaka.
Mechi ya pili ya Taifa Stars katika hatua ya makundi itakuwa Julai 8 mwaka huu dhidi ya Mauritius. Mechi ya mwisho katika hatua hiyo itakuwa Julai 10 mwaka huu dhidi ya Namibia.
Kundi B lina timu za Kenya (Harambee Stars), Botswana (Zebras), Lesotho na Swaziland. Hatua itakayofuata baada ya hapo ni ya mtoano (knockout) na kila kundi litatoa timu moja tu.
Iwapo Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itafuzu kwa hatua itakayofuata itacheza Julai 13 mwaka huu na Afrika Kusini (Bafana Bafana) ambayo pamoja na timu nyingine tano zimekwenda moja kwa moja katika hatua ya mtoano.
Nyingine zilizokwenda moja kwa moja hatua ya mtoano ni wenyeji Zambia, Angola, Zimbabwe, Msumbiji na Malawi ambazo kwenye viwango vya ubora vya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ziko juu ya zile zilizoanzia hatua ya makundi.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo, fainali ya michuano ya Kombe la COSAFA itafanyika Julai 20 mwaka huu.

Sunday, May 5, 2013
Azam vs as far rabat 2-1
Mpira unamalizika kwa Azam kutolewa kwa kufungwa mabao mawili kwa moja.
DK 90: Mwamuzi anaongeza dakika 3 za nyongeza.
DK 88: AS FAR Rabat 2 - 1 Azam FC
DK 82: John Bocco anapiga penati na kukosa
DK 81; Azam wanapata penati baada ya beki wa AS FAR Rabat kuunawa mpira.
DK 80: Azam pamoja na kuwa pungufu wanajitahidi kwenda mbele kujaribu kutafuta bao la kusawazisha - Ameingia Gaudence Mwaikimba.
DK 75: AS FAR Rabat 2 - 1 Azam FC
DK 74: Waziri Omary anapata kadi nyekundu baada ya kumshika mchezaji wa AS FAR Rabataliyekuwa anaelekea langoni mwa Azam.
DK 68: Waziri Omary wa Azam anapewa kadi ya njano kwa mchezo mbaya.
DK 65: Anatoka Brian Umony anaingia Khamis Mcha kwa upande wa Azam
DK 60: Timu zote zinapoteza nafasi kadhaa za kufunga katika kipindi cha dakika 3 zilizopita.
DK 55: Mwamuzi anatoa kadi nyepesi kabisa nyekundu kwa David Mwantika wa Azam
DK 48: Azam bado wanaendelea kucheza kwa kushambulia lango la AS FAR Rabat lakini wanakosa umakini wa kuweza kuingiza mpira kwenye 18 ya wapinzani.
DK 46: Azam wanaanza kipindi cha pili kwa kasi na kufanikiwa kupata ambayo haizai matunda.
Kipindi cha pili kimeanza AS FAR Rabat 2 - 1 Azam FC
Mpira ni mapumziko
DK 45: Mwamuzi anaongeza dakika 3
DK 43: Azam wanafungwa bao la pili hapa -AS FAR Rabat 2-1 Azam
DK 38: Kipre Balou anapewa kadi ya njano - AS FAR Rabat pamoja na kuwa pungufu wanacheza mchezo wa kasi na nguvu.
DK 35: Mchezaji wa AS FAR Rabat anapewa kadi nyekundu kwa kumpiga teke la uso Brian Umony
DK 33: Kipre Tchetche anakosa bao la wazi akiwa amebaki na kipa tu wa AS FAR Rabat
DK 30: AS FAR Rabat wanamiliki mpira kwa muda mrefu huku Azam wakicheza kwa mashambulizi ya kushtukiza
DK 25: Mchezaji yupo akitubiwa baada ya kupata maumivu wakati akizuia shuti liloelekezwa golini kwake
DK 20: A.F.R 1 - 1 Azam FC
DK 12: AS FAR Rabat 1-1 Azam FC. Dakika ya 12 wanasawazisha.
DK 6: Goaaal John Bocco anaipa Azam bao la kuongoza hapa
KICK OFF
1. Mwadini
2. Himidi
3. Waziri
4. Mwantika
5. Atudo
6. Bolou
7. Umony
8. Salum 'sure boy'
9. Bocco (C)
10. Mieno
11. Kipre
Akiba
Aishi
Mwaipopo
Mwaikimba
Abdi Kassim
Mcha Viali
Jabir
Luckson
Sunday, March 10, 2013
Simba sport club leo wamewafunga coastal union 2-1katika uwanja wa taifa jioni hii wakati huo azam fc ikfanya mambo yake na simba sport club inakaribia kuwafikia azam tazama kwa picha zaidi hapa.
Simba sport club leo wamewafunga coastal union 2-1katika uwanja wa taifa jioni hii wakati huo azam fc ikfanya mambo yake na simba sport club inakaribia kuwafikia azam tazama kwa picha zaidi hapa.
Wednesday, February 13, 2013
TIMU YA YOUNG AFRICAN SPORT CLUB LEO IME WAFUNGA AFRCAN LYON KATIKA UWANJA WA TAIFA,MSHAMBULIA JERRY TEGETE LEO KATIKA UWANJA WA TAIFA KAFUNGA MAWILI PEKEEYAKE WAKATI YONG AFRICAN IKIUWA 4-0....
TIMU YA YOUNG AFRICAN SPORT CLUB LEO IME WAFUNGA AFRCAN LYON KATIKA UWANJA WA TAIFA,MSHAMBULIA JERRY TEGETE LEO KATIKA UWANJA WA TAIFA KAFUNGA MAWILI PEKEEYAKE WAKATI YONG AFRICAN IKIUWA 4-0....Monday, February 4, 2013
katika hii picha za taifa stars wakiwa wakijiandaa na mazoezi katika uwanja uliopo dar-es-salaam,wachezaji wote wapo MRISHO KHALFAN NGASSA,MBWANA ALLY SAMATA,THOMAS ULIMWENGU,na wengine.
katika hii picha za taifa stars wakiwa wakijiandaa na mazoezi katika uwanja uliopo dar-es-salaam,wachezaji wote wapo MRISHO KHALFAN NGASSA,MBWANA ALLY SAMATA,THOMAS ULIMWENGU,na wengine.
Subscribe to:
Posts (Atom)